LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 22, 2018

VITA VYA KUWANIA NGAWIRA LIBYA VYAPAMBA MOTO BAINA YA UFARANSA NA ITALIA

Mtandao wa habari wa Algeria umefichua kuwa Ufaransa na Italia zinachuana vikali kuwania ngawira zaidi huko Libya na kwamba wakati mwingine mchuano huo unafikia kiwango cha mapigano na vita vya kisiasa.
Mtandao wa TSA wa Algeria umechunguza taathira za nchi za kigeni nchini Libya na kuandika kuwa, tangu utawala wa Muammar Gaddafi ulipoondolewa madarakani nchini humo, mapigano makali ya kikabila na baina ya makundi ya wanamgambo yamekuwa yakiendelea nchini Libya na kwamba sasa nchi hiyo imekuwa uwanja wa mapigano kati ya Ufaransa na Italia. 
Ripoti hiyo imesema kuwa, hivi karibuni maafisa wa serikali ya Italia waliwatahadharisha wenzao wa Ufaransa kuhusu mwenendo wa kuendelea kuingilia masuala ya ndani ya Libya na jitihada zao za kupeleka mbele mchakato wa kisiasa nchini humo kwa maslahi ya serikali ya Paris.
Rais Macron wa Ufaransa katika "gwanda" la upatanishi Libya
Umeongeza kuwa suala hilo linaonesha kuwa Paris na Rome zinahitilafiana juu ya jinsi ya kusimamia mgogoro wa Libya.
Libya ilitumbukia katika machafuko na vita vya ndani baada ya wanajeshi wa Marekani wakishirikiana na wake wa Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) kuishambulia nchi hiyo na kusaidia harakati za kumuondoa madarakani aliyekuwa kiongozi wa nchi Muammar Gaddafi hapo mwaka 2011. 

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages