Sunday, July 8, 2018

TOT PLUS KUKOLEZA MAPOKEZI YA BIEING 787-8 KWA WIMBO MAALUM, LEO

Baadhi ya wananuziki wa TOT walipokuwa wakijinoa kwa wimbi maalum wa mapokezi ya Ndege mpya aina ya Boeibg 787-8 yatakayofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Kundi la CCM la Tanzania One Theatre (TOT Plus) litanogesha mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner yatakayoongozwa na Rais Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo.

Mkurugenzi wa TOT Gasper Tumaini amesema katika mapokezi ya ndege hiyo Boeing 787-8 Dreamliner kundi hilo litaporomosha wimbo ambao limeutunga maalum kwa ajili ya mapokezi hayo.

Amesema ni wimbo ambao umejaa mistari ya kumpongeza Rais Dk Magufuli na Watanzania kwa jumla kwa kufikia hatua ya kuboresha uchumi wa nchi kwa kuimarisha sekta ya usafiri wa anga.

Ujioo wa Ndege huyo utapanua wigo wa kiushindani wa hali ya juu katika biashara ya Anga,Afrika Mashariki na kati.

Boeing 787-8 itaweka mazingira rafiki kwa Watalii wanaotaka kuja kutembelea Mbuga zetu Serengeti, Ngorongoro,Selous,Manyama,Mikumi bila kusahau kuja kupanda Mlima Kilimanjaro ambao unaweza kuuona hata ukiwa Kenya lakini kuupanda lazima uje Tanzania.

Boeing 787-8 Dreamliner itakata utepe kwa Safari za Mabara China,India,na Ulaya lakini kwanza itachukua Baraka kwa kuruka kwenda Mwanza, Kilimanjaro na hapa Dar es Salaam.

Pia tanzania inatarajia kupokea ndege nyingine kubwa mbili  C300 ambazo zitachanja mbuga kusini mwa Afrika hadi Magharibi mwa Afrika, South Afrika, Zambia, Zimbabwe, Ghana, Nigeria na Congo.

Ikumbukwe kuwa  tayari Bombardier mbili C400 zinafanya vyema kwa kutoa usafiri bora kwa viwango vya Kimataifa na hivyo kufanya wasafiri kupata usafiri wa Uhakika.

Ujio wa Boeing 787-8 Dreamliner utaifanya ATCL sasa kupambana kikamilifu na Mashirika makubwa ya Ndege hapa Afrika kama Ethiopian Airline,Kenya airline na Rwanda Air.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Mdau, andikamaoni yako hapa yasaidie kujua wewe unafikiri nini kuhusu posti hii. Tafdhali, Maoni yako yasiwe ya uchochezi wa aina yoyote.. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

CCM Blog. Powered by Blogger.