Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limelaani hatua ya serikali ya Autralia ya kuwatia nguvuni na kuwafunga wahajiri haramu bila ya tuhuma yotote.
Baraza hilo limetangaza kuwa, baadhi ya wahajiri hao wanashikiliwa katika jela za Australia kwa kipindi cha miezi 9 sasa bila ya kuambiwa tuhuma zao. Baraza hilo limeikosoa Autralia kwa kukanyaga haki za binadamu na kuitaka serikali ya nchi hiyo iheshimu haki hizo na kuwaachia huru wahajiri hao.
Timu ya Umoja wa Mataifa inaloshughulikia ukiukaji wa haki za binadamu tangu mwaka 2017 hadi sasa imetoa ripoti tano ikikosoa vitendo vya kutiwa nguvuni ovyo wahajiri haramu nchini Australia na kulaani vitendo hivyo. Kwa mujibu wa sheria eti ya kukabiliana na wahajiri haramu ya serikali ya Australia, wahajiri wote wanaotaka kuingia nchini humo kupitia njia ya bahari wanapaswa kutiwa nguvuni na kufungwa katika kambi na vituo vilivyoko nje ya nchi hiyo ikiwemo kambi ya Manus huko Papua New Guinea. Mahabusi hao wanaishi katika mazingira mabaya sana na serikali ya Australia imeendeleza mwenendo huo usio wa kibinadamu hususan dhidi ya wanawake na watoto, licha ya malalamiko makubwa ya kimataifa.
Mtaalamu wa haki za binadamu, Elison Betison anasema: "Kuwafunga jela wakimbizi kunakofanywa na serikali ya Australia ni kinyume na sheria na sera hizo zinakinzana na sheria za kimataifa na si za kibinadamu."
Serikali ya Autralia inadai kuwa kurefuka kwa mwenendo wa kuwashikilia wakimbizi kunatokana na taratibu za kiidara na si kuwaadhibu watu hao. Hata hivyo duru za sheria za kimataifa zinaamini kuwa, serikali ya Australia imezifanya kambi na vituo vya kuwashikilia wahajiri na wakimbizi kuwa machinjio ya watu hao, suala ambalo ni uhalifu na jinai na linapaswa kukomeshwa haraka iwezekanavyo.
Vilevile mtaalamu wa masuala ya kijamii wa Australia McKim anasema: Mienendo kama hii dhidi ya wakimbizi na wahajiri nchini Australia inakiuka haki za binadamu, na serikali ya nchi hiyo inapaswa kuwajibika kama ilivyotakiwa na Umoja wa Mataifa."
Inasemekana kuwa, karibu wakimbizi na wahajiri elfu mbili wanashikiliwa katika kambi na mahabusu zilizoko kwenye visiwa vya Nauru na Manus katika bahari ya Pacific, na 150 miongoni mwao ni watoto wadogo. Kwa kutilia maanani makubaliano yaliyofikiwa hivi karibuni kati ya serikali za Marekani na Autralia pia kuhusu kuhamishia nchini humo baadhi ya wahajiri, tunaweza kusema kuwa serikali ya Autralia inaamiliana na wakimbizi na wahajiri hao kama watumwa wanaoweza kuuzwa na kununuliwa. La kusikitisha zaidi ni kuwa jumuiya kubwa za kimataifa hazijachukua hatua ya maana ya kukomesha ukatili huo na zimetosheka kutoa taarifa na matakwa yasiyo na dhamana ya utekelezaji.

No comments:
Post a Comment
ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇