BREAKING NEWS

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, July 27, 2018

NAIBU WAZIRI WA NISHATI SUBIRA MGALU ATOA MAAGIZO KWA TANESCO KUHUSU MRADI WA REA

  NA MWANDISHI MAALUM, MTWARA

NAIBU Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu (aliyeshika mkasi) ameliagiza shirika la Umeme Tanzania Tanesco kuhakikisha vijiji vyote vinavyopitiwa na mradi wa REA vinapatiwa umeme haraka na kuachana na mwenendo wa kusuasua Ili wananchi waendane na fursa zilizopo.
Ametoa agizo hilo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya REA katika halmashauri ya mji wa Nanyamba Mkoani Mtwara na kuzindua mradi huo katika kata ya Nalingu halmashauri ya wilaya ya Mtwara.

Akiwa Nalingu Mhe. Naibu waziri Subira amesema uwepo wa gesi asilia katika halmashauri ya Mtwara umesaidia vijiji vingi nchini kunufaika lakini hasa mkoa wa Mtwara kwani serikali inajenga kituo cha kuzalisha umeme wa Gas Megawat 300.

 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, akihutubia wananchi.
 Wananchi wakisikiliza hotuba ya Mhe. Subira Mgalu.
 Picha ya pamoja baada ya kuwasha umeme.
Mwananchi akitoa maoni yake

No comments:

Post a Comment

Mdau, andikamaoni yako hapa yasaidie kujua wewe unafikiri nini kuhusu posti hii. Tafdhali, Maoni yako yasiwe ya uchochezi wa aina yoyote.. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages