LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 9, 2018

NAIBU WAZIRI NDITIYE AFUNGUA MKUTANO WA UMOJA WA TAASISI ZA POSTA KWA NCHI WANACHAMA WA KUSINI MWA AFRIKA (SAPOA) JIJINI DAR ES SALAAM

Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi na Mawasiliano), Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kulia), akiwa meza kuu pamoja na baadhi ya wawakilishi wa Umoja wa Posta kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SAPOA), katika mkutano wa umoja huo, alioufungua leo, ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwan'gombe na wa pili ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Shirika la Posta Tanzania, Elia Madulesi akizungumza katika mkutano huo, kabla ya kuwakaribisha wawakilishi wa Umoja wa Posta kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SAPOA), kuzungumza katika mkutano huo.
Baadhi ya wawakilishi kutoka DHL, ambao ni wafadhili wa mkutano huo, wakifuatilia maelezo mbalimbali kutoka kwa wawakilishi wa nchi mbalimbali za umoja huo.
Wawakilishi kutoka Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakiskiliza kwa makini maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na wawakilishi wa nchi za umoja huo, wakati wa  ufunguzi wa mkutano huo. Kutoka kushoto ni Kaimu Meneja Uendeshaji wa Biashara, Mwanaisha Saidi, Kaimu Meneja Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo na Meneja Huduma za Fedha, Rehema Mbunda.
Wawakilishi kutoka Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakifuatilia mkutano huo. 
Baadhi ya wawakilishi kutoka nchi za Kusini mwa Afrika zilizounda umoja huo, wakifuatilia kwa makini hotuba na maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa katika mkutano huo.
Baadhi ya wawakilishi wa umoja wa SAPOA, kutoka nchi za Kusini mwa Afrika, wakifuatilia kwa makini mkutano huo.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa umoja huo, Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu J.K. Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Posta wa Mauritius, Giandev Moteea, akitoa hotuba yake katika mkutanoni huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo akitoa hotuba yake katika ufunguzi wa mkutano huo, wa umoja wa Posta kwa nchi zilizomo Kusini mwa Afrika (SAPOA), jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Umoja wa Posta (SAPOA), katika Ukumbi wa  Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam leo. 
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta akifafanua masuala mbalimbali kwa waandishi wa habari, mara baada ya kutoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo. 
Maofisa wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha TPC, Elia Madulesi (kulia) na Joseph Ngowi (kushoto), wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa ukitolewa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta kwa waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati), akiwa na Mtendaji Mkuu wa Posta nchini, Mauritius Giandev Moteea (wa nne kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta (TPC), Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo (wa nne kulia), Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta, Hassan Mwang'ombe (wa tatu kulia), katika picha ya pamoja na baadhi ya wawakilishi kutoka nchi mbalimbali zilizo katika Umoja wa Posta kwa nchi zilizo ya Kusini mwa Afrika (SAPOA), jijini Dar es Salaam leo. 

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages