Tuesday, July 10, 2018

MAPIGANO KATI YA JESHI LA UGANDA NA KONGO DR YASHTADI ZIWA EDWARD, WAVUVI 12 WAUAWA

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesema wavuvi wasiopungua 12 raia wa nchi hiyo wameuawa katika mapigano makali yanaoendelea kushuhudiwa kwa siku kadhaa sasa kati ya vikosi vya majini vya nchi hiyo na Uganda, katika maji ya Ziwa Edward.
Muhindo Kyakwa, afisa mwandamizi wa DRC katika eneo la Kivu Kaskazini ameliambia shirika la habari la AFP kuwa, "Miili ya raia wetu 12 ingali inaolea katika maji ya Ziwa Edward, baada ya makabiliano makali baina ya askari wa majini wa Uganda na Kongo DR. Tumeshindwa kuziopoa maiti hizo kwa kuwa wanajeshi wa Uganda wanamfyatulia risasi mtu yeyote anayekaribia eneo hilo."
Awali serikali ya Kinshasa ilikuwa imedai kuwa, wavuvi 16 raia wa Kongo wametoweka katika maji ya Ziwa Edward.
Alkhamisi iliyopita, askari wanne na raia watatu wa Uganda waliripotiwa kuuawa katika mapigano hayo baina ya vikosi vya majini vya Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika maji ya Ziwa Edward.

Wavuvi wa Uganda katika Ziwa Edward

Hujuma hiyo ilifanyika chini ya masaa 48 baada ya kikosi cha majini cha Uganda kuwatia mbaroni wavuvi 18 raia wa Kongo kikidai kuwa walikuwa wameingia katika maji ya nchi hiyo ndani ya Ziwa Edward.
Watu wasiopungua 30 aghalabu yao wakiwa wavuvi wanahofiwa kupoteza maisha katika makabiliano hayo baina ya wanajeshi wa majini wa Uganda wa DRC katika maji ya Ziwa Edward lililoko katika mpaka wa nchi mbili hizo jirani.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Mdau, andikamaoni yako hapa yasaidie kujua wewe unafikiri nini kuhusu posti hii. Tafdhali, Maoni yako yasiwe ya uchochezi wa aina yoyote.. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

CCM Blog. Powered by Blogger.