Tuesday, July 10, 2018

KUONGEZEKA UKOSOLEWAJI WA SIASA ZA TRUMP KUHUSIANA NA SUALA LA KOREA KASKAZINI

Sambamba na kuanza tena vita vya maneno kati ya Marekani na Korea Kaskazini, ukosolewaji wa siasa za Rais Donald Trump kuhusiana na jinsi amekuwa akiamiliana na Korea Kaskizini umekuwa ukiongezeka.
Seneta Chris Coons wa chama cha Democrat cha nchini Marekani anasema kwa mtazamo wake, mazungumzo ya viongozi wa nchi mbili hizo huko Singapore mwezi uliopita yalikuwa ni maonyesho tu ya televisheni  ambayo hayakuwa na lengo jingine isipokuwa kwa ajili ya viongozi hao kupeana mikono. 

Anaendelea kusema kuwa hii ni katika hali ambayo Rais Donald Trump wa Marekani aliamua kufutilia mbali manuva ya pamoja ya kijeshi na Korea Kusini bila ya kushauriana na washirika wake wa eneo na hivyo kutopata faida yoyote kutokana na hatua hiyo.

 Ukosoaji huo unatolewa katika hali ambayo, vita vya maneneo kati ya Marekani na Korea Kaskazini vilianza tena tarehe 8 Julai baada ya vita hivyo kusitishwa kwa wiki kadhaa. 

Afisa mmoja wa Korea Kaskazini alitaja matakwa ya Marekani yaliyowasilishwa kwa nchi hiyo katika safari ya Mike Pompeo, Waziri wa Marekani huko Pyongyang, mji mkuu wa Korea Kaskaini kuwa ni ya 'kijambazi', 

Naye Pompeo kukosoa matamshi ya afisa huyo wa Korea Kaskaizni, alipowasili mjini Tokyo Japan, kuwa matakwa hayo ambayo alidai kuwa ni ya jamii ya kimataifa hayakuwa ya kijambazi.

Seneta Chris Coons wa chama cha Democrat

wakati huohuo Lindsey Graham, seneta mwingine wa Marekani wa chama cha Republican, amesema kwamba ahadi aliyoitoa Trump kupitia ujumbe wake wa Twitter kuwa dunia ingelala usingizi mnono baada ya mazungumzo yake na  Kim Jong-un, kiongozi wa Korea Kaskazini huko nchini Singapore, sasa imewakosesha usingizi viongozi wa nchi hiyo ya Asia Mashariki. Kwa vyovyote vile inaonekana kuwa stratijia ya Trump kupata fursa kutoka kwa Korea Kaskazini na wakati huohuo kutotoa fursa yoyote kwa nchi hiyo imegonga ukuta. Viongozi wa Korea kaskazini wanasisitiza kuwa kutokomezwa silaha za nyuklia katika Peninsula ya Korea Kaskazini kunapasa kwenda sambamba na kuondolewa vikwazo vyote vilivyowekwa dhidi ya nchi hiyo. Hii ni katika hali ambayo watawala wa Marekani wanasisitiza kwamba vikwazo hivyo havitaondolewa hadi pale watakapohakikisha kwamba silaha zote za nyuklia za Korea Kaskazini zimetokomezwa. Viongozi wa Korea Kaskazini wanasema kuwa mtazamo huo wa Marekani ni wa kijambazi, ibara ambayo ni kali zaidi kuwahi kutumiwa na viongozi hao tokea kufanyika mazungumzo kati ya Kim Jong-un na Trump nchini Singapore.

Trump akipeana mkono na Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini walipokutana nchini Singapore

Moto wa vita vya maneno kati ya Washington na Pyongyang umeanza kuwaka tena katika hali ambayo Trump amekuwa akizungumzia mafanikio yake katika kuilazimisha Korea Kaskazini kuharibu silaha zake za nyuklia. Katika jumbe zake nyingi ambazo amekuwa akizituma mara kwa mara kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, Trump amekuwa akijinadi kuwa shujaa wa kutokomezwa silaha za nyuklia za Korea Kaskazini na hivyo eti kuokoa jamii ya mwanadamu kutokana na vita vya atomiki katika eneo la Asia Mashariki. Ni wazi kuwa kuepushwa vita vya atomiki kati ya Marekani na Korea Kaskazini utakuwa ni ushindi mkubwa kwa Donald Trump na chama chake cha Republican ambacho kinatarajiwa kuchuana vikali na chama pinzani cha Democratt katika uchaguzi mdogo ujao wa Congress unaotarajiwa kufanyika nchini Marekani hivi karibuni.

Kombora la kwanza la ICBM la Korea Kaskazini

Kama Trump atashindwa kufikia lengo hilo, ni wazi kuwa hilo litakuwa ni pigo kubwa kwake kama mtu binafsi na pia kwa chama chake cha Republican katika uchaguzi huo, suala ambalo huenda likapelekea wapinzani wake kuchukua uongozi wa Conress. Ni kwa kuzingatia suala hilo ndipo licha ya kuwepo tofauti kubwa kati ya pande mbili lakini bado Trump anaendelea kuzungumzia mafanikio ya mwenendo wa kutokomezwa silaha za nyuklia za Korea Kaskazini, suala ambalo linatazamwa na Seneta Chris Coons wa chama cha Democrat kuwa maonyesho tu ya televisheni ambayo yamepangwa kwa ajili ya viongozi wa nchi mbili hizo hasimu kupeana mikono.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Mdau, andikamaoni yako hapa yasaidie kujua wewe unafikiri nini kuhusu posti hii. Tafdhali, Maoni yako yasiwe ya uchochezi wa aina yoyote.. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

CCM Blog. Powered by Blogger.