Monday, July 16, 2018

JESHI LA NIGERIA LATANGAZA KUUA MAGAIDI 22 WA BOKO HARAM

Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa limeua magaidi 22 wa kundi la Boko Haram katika mapigano makali kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Katika taarifa leo Jumatatu, Jeshi la Nigeria limesema mapigano hayo yalijiri katika eneo la Bama jimboni Borno wikiendi hii ambapo magaidi kadhaa wa Boko Haram wametoroa wakiwa wamejeruhiwa.
Taarifa hiyo pia imesema wanajeshi wawili wamejeruhiwa katika oparesheni hiyo.
Wakati huo huo Jeshi la Nigeria limekanusha taarifa kuwa askari wake 23 wametoweka baada ya kambi yao kushambuliwa na magaidi wa Boko Haram.
Mkuu wa Mahusiano ya Umma katika jeshi hilo Brigedia Jenerali Texas Chukwu amesema ripoti hiyo ilmetiwa chumvi huku akidai kuwa Jeshi la Nigeria linadhibiti hali ya mambo.
Awali afisa wa jeshi ambaye hakutaka jina lake litajwe aliliambia shirika la habari la AFP kuwa, hatima ya wanajeshi 23 wakiwemo watano wa akiba haijulikani kufikia sasa, baada ya wanachama wa Boko Haram kuvizia na kuvamia msafara wa magari ya jeshi la nchi hiyo mjini Maiduguri, makao makuu ya jimbo la Borno.
Amesema shambulizi hilo lilitekelezwa na wanachama zaidi ya 100 wa Boko Haram katika kijiji cha Balagallaye, eneo la Boboshe nje kidogo ya mji wa Bama.
Zaidi ya watu elfu 20 wamepoteza maisha nchini Nigeria tokea kundi la magaidi wakufurishaji wa Boko Haram lianzishe uasi mwaka 2009, huku wengine zaidi ya milioni mbili wakilazimika kukimbia makazi yao kutokana na ugaidi wa kundi hilo ambao sasa umeenea katika nchi jirani kama vile Cameroon, Niger na Chad.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

CCM Blog. Powered by Blogger.