LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 29, 2018

HATIMAYE AHED TAMIMI, MSICHANA ALIYEPAMBAN NA ASKARI WA KIZAYUNI AACHIWA HURU

Utawala haramu wa Kizayuni umewaachilia huru Ahed Tamimi, msichana wa Kipalestina na mama yake Nariman baada ya kuwaweka kizuizini kwa kipindi cha miezi minane.
Ahed Tamimi alitiwa nguvuni tarehe 19 Disemba mwaka jana na utawala huo katili. Kosa pekee lililokuwa linamkabili msichana huyo wa Kipalestina mwenye umri wa miaka 17, ni kupambana na askari wa Kizayuni akitaka kuwaondoa katika uwa wa nyumba yao. Kufuatia kutiwa mbaroni msichana huyo shupavu, katika miezi ya hivi karibuni, miji mbalimbali ya dunia ilishuhudia maandamano ya wananchi ya kumuunga mkono Tamimi.
Wakati Ahed Tamimi, alipokuwa akishikiliwa na utawala katili wa Kizayuni
Aidha Umoja wa Ulaya na asasi mbalimbali za kimataifa na za haki za binaadamu, ziliukosoa vikali utawala huo haramu wa Kizayuni kwa kumkamata binti huyo. Kwa upande mwingine, kituo cha kufuatilia masuala ya mateka na wafungwa wa Kipalestina wanaozuiliwa katika utawala haramu wa Kizayuni, kimetangaza kwamba, katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo ya mwaka huu, askari wa utawala huo wamewatia nguvuni zaidi ya Wapalestina 1000 katika mji wa Quds pekee.
Ahed Tamim, msichana shupavu wa Kipalestina
Riyad Ashqar, Msemaji wa kituo hicho amesema kuwa, katika kujaribu kuzima harakati na maandamano ya Wapalestina kufuatia uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani wa kuutangaza mji wa Quds kuwa mji mkuu wa utawala haramu wa Israel na kadhalika hatua yake ya kuhamisha ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv kwenda mji huo, askari wa Kizayuni walianzisha kamatakamata kubwa dhidi ya Wapalestina wa maeneo ya Quds. Hii ni katika hali ambayo hadi sasa karibu Wapalestina 7000 wanaendelea kushikiliwa katika jela 22 za utawala huo katili. Kati yao ni wanawake na wasichana 63, watoto 350 na wabunge 12.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages