LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 22, 2018

CHINA YASISITIZA KUKABILIANA NA VITISHO VYA KIBIASHARA VYA MAREKANI

Wizara ya Mambo ya Nje ya China na katika radiamali yake juu ya vitisho vya Rais Donald Trump wa Marekani kuhusiana na kuziwekea ushuru wa zaidi ya Dola bilioni 500 bidhaa za China zinazoingizwa nchi yake, imesema kuwa Beijing haitosalimu amri mbele ya mashinikizo na vitisho vya Washington.
Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imekosoa vitisho vya kibiashara vya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya China na kusema kuwa Beijing inaamini kwamba vita hivyo vya kibiashara havitakuwa na mshindi na kwamba Marekani katika njia hiyo ya hatari itawasababishia madhara raia na mashirika ya nchi hiyo.
Wizara ya Mambo ya Nje ya China imeongeza kwamba, ushuru ulioongezwa na Marekani kwenye sekta ya biashara pamoja na vitisho ni hatua zisizo na busara na mantiki kama ambavyo pia hazihalalishiki na kwa sababu hiyo China itakabiliana na Marekani katika uwanja huo.




Vita vya kibiashara kati ya China na Marekani

Hivi karibuni pia Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China aliikosoa vikali Marekani kwa kuanzisha vita vya kibiashara duniani. Akizungumza na waandishi habari mjini Beijing, Hua Chunying alisema kuwa, vita vya kibiashara vilivyoanzishwa na Marekani si tu kuwa vitapelekea China ihasimiane na Marekani bali pia vitasababisha kuongezeka uhasama baina ya Washington na mataifa mengine mbali na kusababisha matatizo ya kiuchumi duniani.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages