LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 6, 2018

CCM MWAMBA: TWAWEZA

Na Jerry C. Muro
Wasalamu, nimeona niseme Jambo katika Kuchambua kidogo utafiti Uliotolewa jana na Twaweza naandika kwa Kuchukua baadhi ya taarifa muhimu za Wachangiaji Wengine katika Mjadala huu.

Ukweli ni kwamba TAKWIMU za utafiti wa TWAWEZA zina habari MBAYA ZAIDI kwa UPINZANI kuliko kwa CCM. Lakini kwa vile upinzani hauna mazoea ya KUJITAFAKARI na kujipanga upya, WANAPOTEZA muda wote kukodolea takwami upande wa CCM.

 TWAWEZA wanaonesha kwamba hata kama UCHAGUZI utafanyika leo, CCM WATASOMBA Serikali za Mitaa na Vijiji, Udiwani na URAIS!!! Tena, CCM bado ina wingi ule ule wa wanaokipenda tokea uchaguzi uliopita (2015). THELUTHI MBILI za waliohojiwa wanakipenda CCM. Hivyo CCM bado IMARA zaidi ya vyama vya Upinzani.

Mbaya zaidi ni kwamba *TWAWEZA* wanaonesha kuwa chama cha *Zitto Kabwe (ACT), *HAKINA* Umaarufu wowote wa maana. Lakini yeye anakazana kukemea mambo ambayo kichama hayawezi kumuongezea kura kwenye chama chake. Hivyo anapoteza pumzi kwenye masuala yasiyo na mashiko kwa wapiga kura kichama. *CUF* nacho hali yake si ya kujivunia hata kidogo.

Takwimu za *TWAWEZA* zinaonesha kwamba kuna tabaka linaloongezeka kwa kasi, nalo ni lile la wananchi wanaotoka zaidi kwenye upande wa upinzani na kuhamia kwenye kundi lisilo na chama. Hapa *CCM* imepoteza asilimia ndogo zaidi ya wanaokipenda, kuliko ilivyo kwa Chadema. Hapa unaweza kusema Chadema na upinzani unakimbiwa kwa kasi, na ingawa hawakimbilii CCM, lakini wanaowapoteza wapambe katika hama hama hii ni upinzani zaidi.

Kuhusu suala la umaarufu wa Rais, hili si tatizo kwa *CCM* .Unaweza kusema hivi kwa maana bado CCM kinapendwa na asilimia 60 ya waliohojiwa. Pia CCM wapiga kura wake ni aina ile ya watu wasiokubali kuyumbayumba kirahisi, yaani watu wa umri mkubwa na walioona mengi kwa miongo zaidi ya 5, na ambao hawadanganyiki na siasa za kileo. Hao vijana wa umri wa miaka 18 hadi 29, bado kawaida ni vigeugeu na bado hawana uzoefu mkubwa kimaisha kujua mbivu na mbichi.

 *Hitimisho* ni kuwa, *TWAWEZA* wanaonesha bado CCM inapeta, na itaendelea hivyo kwa muda mrefu ujao, hususan kwa kuzingatia ushahidi wa kitakwimu kwamba upinzani unasinyaa na kupoteza dira na ushawishi kwa sehemu kubwa ya wananchi walioupenda miaka 3 iliyopita. Huu ndiyo ujumbe ambao wapinzani wanatakiwa kuukazia macho kwenye utafiti huu wa *TWAWEZA* …

Ukisoma Maandiko Ya *Bw Shillatu* , utaona ameorodhesha mambo mengi ambayo Serikali ya *CCM* imeyafanya tangu kuingia kwa Mhe Magufuli madarakani.

Kwa sasa Ushindani hauko Kati ya CCM na vyama vya upinzani la hasha, Bali Ushindani upo kati YA *CCM* na *WANANCHI* ambao ndio wanapokea Huduma za jamii, ambao ndio wanapokea miradi lukuki inayotekelezwa na Serikali ya *CCM* na mwisho wa Miaka 5 wananchi watasema nini kimefanywa na Sio *Computer* za *Twaweza* .

Wasalamu
 *Jerry C. Muro*
 *06/07/2018*

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages