LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 21, 2018

MOI YAKWANZA KUBUNI MKAKATI MPYA UTOAJI HUDUMA

Mkurugenzi Mtendaji wa Taaasisi ya Mifupa  (MOI) Dkt Respicious Boniface (wapili kushoto) akifungua mafunzo ya wataalamu 12 wakubeba wagonjwa 'patient Transporters’ ambayo yamefanyika katika Taasisi hiyo Julai 20, 2018. Mafunzo hayo yamehusisha ‘Basic life support ‘ yaliyofanyika kwa miezi 6, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Tiba katika Taasisi hiyo Dokt. Samuel Swai na wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi, Fidelis Minja.




Mkurugenzi Mtendaji wa Taaasisi ya Mifupa  (MOI) Dkt. Respicious Boniface (wa tatu kulia) katika picha ya pamoja


Wahitimu wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja








Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi, Fidelis Minja, akizungumza na kuwaomba wauguzi, Tutoe huduma Bora kwa wagonjwa wetu ambayo huduma hii itaweza kuwa na matarajio ya kukamilisha malengo ya Taasisi tuwape ushirikiano wahitimu wetu 






Mkurugenzi Mtendaji wa Taaasisi ya Mifupa  (MOI) Dkt. Respicious Boniface (wapili kushoto) akimkabidhi sare maalum, Sheha Juma Sheha mara baada ya kufungua mafunzo ya wataalamu 12 wakubeba wagonjwa 'patient Transporters’ ambayo imefanyika katika Taasisi hiyo, Julai 20, 2018 mafunzo hayo yajulikanayo kama ‘Basic life support ‘ yaliyofanyika kwa miezi 6, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Tiba katika Taasisi hiyo Dokt. Samuel Swai na wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi, Fidelis Minja 

Mkurugenzi Mtendaji wa Taaasisi ya Mifupa  (MOI) Dkt Respicious Boniface (wapili kushoto) akimkabidhi sare maalum, Deogratius Mapunda mara baada ya kufungua mafunzo ya wataalamu 12 wakubeba wagonjwa 'patient Transporters’ ambayo imefanyika katika Taasisi hiyo, Julai 20, 2018 mafunzo hayo yajulikanayo kama ‘Basic life support ‘ yaliyofanyika kwa miezi 6, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Tiba katika taasisi hiyo Dokt. Samuel Swai na wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi, Fidelis Minja 


Mkurugenzi wa Tiba katika Taasisi ya Mifupa (MOI) Dokt. Samuel Swai (kushoto) akizungumza jambo katika hafla hiyo, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa  (MOI) Dkt. Respicious Boniface.


 Niwashukuru vijana kwa kuwapongeza kuhitimu mafunzo na wakiwa na moyo wa kujituma, kwa kuwa na Lugha nzuri kwa wagonjwa na wakiwa na ufanisi mkubwa pili niupongeze uongozi uliotowa wazo, kwani 'patient Transporters’ wapo Dunia nzima na nitaaluma, ila limekuja jambo hili kwa uzuri kabisa hawa wamepatikana wana moyo na watakao wakwamisha hawa nijana watapata tabu sanaaa!. tusipo badilika tutapata tabu sanaa! 


Baadhi ya Mameneja walio hudhuria










Kaimu meneja wa Jengo, Elizabeth mbaga akikaribisha viongozi mbalimbali waliofika pamoja na wafanyakazi wakiwemo wahitimu wa mafunzo hayo


Afisa Muuguzi wodi ya majeruhi ya akina mama, Loema Nzugika akipongeza Uongozi wa Uuguzi na Mameneja wote akiwemo kiongozi wa chumba cha upasuaji  kwa kuweza kubuni mpango mkakati wa kuboresha huduma hiyo, pamoja na namba ndogo ya upungufu wa wafanya kazi ilikuwa inatuwia vigumu kutekeleza kazi zetu ila kwa mpango huo hakika imeturahisishia sana kupunguza mgonjwa kukaa sana mara amalizapo kupatiwa huduma kutoka katika chumba cha upasuaji au kuchukuliwa kutoka wodini na  kwenda katika chumba cha upasuaji, mwisho niwapongeze wahitimu kwani wamekua msaada mkubwa sana na wamepunguza changamoto kubwa na wameongeza ufanisi wa kazi zetu na tuweze kumpa ushirikiano Kaimu Mkurugezi wa Uuguzi 


Kaimu Meneja wodi za kulipia, Maagreth kumpuni akianza kwa kumshukuru Mungu na kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji na viongozo wote waliofika katika hafla hiyo na  kumpongeza Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi pamoja na viongozi wa Uuguzi wote kwa kushirikiana vyema katika kumsaidia kazi Mkurugenzi wa Uuguzi,   Hakika napenda kumpongeza Kaimu Mkurugenzi kwa kuliweka mezani jambo hili na kulichambua na kuangalia ni yapi ya kupunguza na yapi ya kuongeza na leo hii tunayaona matunda yake, alisema Kumpuni,  (MOI) Oyee, na kuitikiwa Oyee na pia niwapongeze pia na wahitimu ambao wamekuwa bega kwa bega na nikiwa na uhakika wameyashika yale waliyo fundishwa na wapo vizuri, Changamoto ndogondogo tutaendelea kuzitatua na  shukuru kwa kipindi hiki hakujatokea janga ambapo ingelikuwa kashfa kwa Taasisi na Mungu ametuwezesha hapajatokea janga lolote, hivyo kwa ushirikiano wao mzuri tuendelee kuwapa ushirikiano zaidi ili (MOI) izidi kusonga mbele.  
Capten, Adam Leyna (kushoto) ambaye ni Mwenyekiti wa Wauguzi Saccos Tanzania pia ni Muuguzi wa Hospitali ya Lugalo kitengo cha upasuaji kwa upande wa nusu kaputi akizungumza jambo, wakwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taaasisi ya Mifupa  (MOI) Dkt. Respicious Boniface na Mkurugenzi wa Tiba wa Taasisi hiyo Dokt. Samuel Swai.


MOI yakwanza katika kubuni mpango mpya wa utoaji huduma upande wa mahospitalini, hayo aliyasema,  Capten Leyna kabla ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taaasisi ya Mifupa  (MOI) Dkt. Respicious Boniface  kufunga mafunzo ya wataalamu 12 wakubeba wagonjwa 'patient Transporters’ ambayo yamefanyika katika Taasisi hiyo Julai 20, 2018 mafunzo hayo yajulikanayo kama ‘Basic life support ‘ yaliyofanyika kwa miezi 6, aliendelea kusema Caten Leyna.



   Napenda kutoa pongezi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya (MOI) na viongozi wote, Pia nimpongeze Kaimu Mtendaji wa Uuguzi kwa kubuni wazo kama hili.


Hakika wauguzi wenzangu tuanze na slogan yetu, 

Tusifanye kazi kwa mazewea, laasivyo watapata tabu sanaa.

Mkurugenzi mtendaji kutokana na umuhimu wa tukio hili sikupenda kutuma hata mwakilishi kutokana na kubuni mkakati ambao katika Hospitali zote zinazotoa huhuduma za kiafya (MOI) imekua yakwanza kubuni huu mkakati na kutoa huduma hii.


Ninaamini kama imekuwa yakwanza katika kuleta tija ya namna hii basi cheche hizi zitasambaa nchi nzima na mimi naanza kuondoka nayo hii.


Hivyo niwapongeze na nimpongeze Kaimu Mkurugenzi wa Uuguzi kwa wazo hili na hatua ambazo ulizoweza kuthubutu kuwa hatua uliyochukua kuwa mamoja na wenzako. 


Sasa wazo hili lilipokuja kwetu kwenye bodi ukweli kwamba tulikaa na viongozi wengine tukalichambua lakini tukaona kwamba sisi kama wauguzi Saccos Tanzania niwadau wakubwa wa Taasisi ya Mifupa (MOI), na nikwa nini ni wadau kwanza, Kaimu Mkurugenzi wa Uuguzi MOI ni Mjumbe wa Bodi ya Wauguzi Saccos, pili ni mwenyekiti wa kamati ya mikopo ya wauguzi Saccos Tanzania. 


Hivyo kamati iliona ifadhili Sare za wahitimu hao 12 ambazo zitakazo watambulisha katika muonekano ulio mzuri na thamani yake ni 400,000. 


Tutaendelea kufadhili kama ikakavyo wezekana, pia pamoja na kufadhili nitowe wito kwa wauguzi wenzangu tukitumie chama hiki cha Wauguzi Saccos, naweza kuwapa historia fupi ya jinsi chama hiki kilivyoanza na  sasa hivi kilipo.


Kilianza na wanachama 21 wakati kinaanza kusajiliwa, Novemba  2014 na hivi ninavyo zungumza sasa hivi kinawanachama zaidi ya 15000 na tunamtaji zaidi ya Mil. 400 na tumeisha koposha zaidi ya mil. 250 pesa ambayo ipo  mikononi mwa wauguzi, Capten, Leyna aliendelea kusema. 


Wauguzi naomba niseme, Kaimu wa Huduma za Uuguzi anaweza kuwaonyesha hata ujumbe mfupi katika simu yake kutok kwa mwanacha mwezetu ambaye kwa sasa yupo Misri na familia yake ikapata shida ipo hapa Tanzania lakini tulimtumia fomu na akazirejesha kwa wakati na ndani ya siku 3 ameushukuru uongozi na wanacha kwa kupata mkopo wa ada ya familia yake, kiasi cha Sh. mil. 200. 


Haijalishi upo umbali gani na mwisho wa malipo hayo ya ada ilikuwa Julai 20, 2018, hivyo napenda niseme huwezi ijuwa radha yake kwa sababu upo nje ila ingia uone kile tunancho kimaanisha na ndani ya miaka michache tunahitaji kubadilika katika jina la kukopeshana na tuwe na Benk iyakayo julikana  Wauguzi Benk Saccos Tanzania. 


Hivyo napenda kusema asanteni sana kwa kunialika na kuushukuru uongozi mzima wa Taasisi ya Mifupa MOI kwani kunakitu hapa nimejifunza.


   



Baadhi ya viongozi wakisikiliza kwa umakini wakati, Capten, Adam Leyna alipokuwa akizungumza
(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages