LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 27, 2018

RAIS MNANGAGWA KUTUA NCHINI KESHO

Na Immaculate Makilika-MAELEZO
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa (Pichani) anatarajiwa kufanya ziara ya siku mbili nchini kuanzia Juni 28 hadi  29 ikiwa ni mara ya kwanza kuja nchini tangu aingie madarakani Novemba 2017.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imesema lengo la ziara hiyo ni kujitambulisha kwa Rais na wananchi wa Tanzania.
"Ziara hii ni muhimu kwa Tanzania kwani itatoa fursa ya kuimarisha na kukuza zaidi mahusiano mazuri yaliyopo ya kidiplomasia, kihistoria, kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizi mbili. 

Pamoja na kutoa fursa kwa viongozi wetu kujadili masuala mbalimbali yanayohusu nchi hizi mbili ya kikanda na Kimataifa", taarifa hiyo imesema.

Taarifa imesema, wakati wa ziara hiyo,   Rais Mnangagwa atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli.

Rais Mnangagwa anatarajiwa kutembelea Chuo cha Sanaa cha Kaole Bagamoyo ambacho awali kilitumika kutoa mafunzo kwa wapigania uhuru kutoka nchi za Kusini mwa Bara la Afrika. Ambapo  Rais Mnangagwa ni miongoni mwa waliopata mafunzo katika chuo hicho.

Aidha, tangu aingie madarakani Rais Mnangagwa ameshafanya ziara katika nchi za Namibia, Zambia, Msumbiji, Angola, Afrika Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Botswana.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages