Sunday, March 11, 2018

CCM Z'BAR YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA KADA WAKE

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mzee Abdulrazaq Mussa Simai 
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’, ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Kada wake marehemu Mzee Abdulrazaq Mussa Simai 'Kwacha' aliyefariki  leo Machi 11,20118.

Mzee  Abdulrazaq  amefariki katika  Hospitali ya Kuu ya Taifa ya Muhimbili, iliyopo  Jijini Dar es salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Katika Salamu hizo Dk. Mabodi amesema CCM imepokea taarifa ya kifo hicho kwa  mshutuko mkubwa na uzuni ya hali ya juu, kutokana na  marehemu Abdulrazaq alikuwa mwadilifu kwa Chama chake na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wote wa uhai wake, na amemtaja kuwa ni miongoni mwa Wana ASP aliyeyalinda na kuyathamini Mapinduzi ya mwaka 1964 kwa vitendo.

Kupitia salamu hizo Dk. Mabodi amewaomba  familia ya marehemu, Wanachama, Viongozi na Watendaji wote wa CCM, Marafiki, Ndugu  na Jamaa wote walioguswa na msiba huu kuwa na subra katika kipindi hiki kigumu  na kuendelea  kumuombea dua.

Enzi za uhai wake Abdulrazaq amewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Chama na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ikiwemo Katibu Maalumu wa aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Aman Karume.

Marehemu amezikwa leo katika kijiji cha Paje wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja, amefariki akiwa na umri wa miaka 98 ameacha watoto watano  na  kizuka mmoja. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu pahala Pema Peponi Amin.

Imetolewa na ;
   
Catherine Peter Nao
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,
Idara ya Itikadi na Uenezi CCM,
ZANZIBAR,

11 Machi,  2018.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Mdau, andikamaoni yako hapa yasaidie kujua wewe unafikiri nini kuhusu posti hii. Tafdhali, Maoni yako yasiwe ya uchochezi wa aina yoyote.. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

CCM Blog. Powered by Blogger.