Tuesday, February 27, 2018

UJUMBE WA WAZI KWA RAIS DK JOHN MAGUFULI

NA JOSEPH YONA
Rais wetu mpendwa, kwanza kabisa pole na safari, safari ambayo naamini kuna matumaini yajayo katika taifa letu, kupitia Jumuiya zetu hizi za Afrika Mashariki na Kati.

Bahati nzuri Nilifuatilia kwa karibu mizunguko yako na Hotuba zako zoote kupitia kwa Mkurugenzi wetu wa Mawasiliano IKULU Gerson Msigwa.

Rais wetu mpendwa lengo la waraka huu no 1 kutoka kwangu Mtanzania Mnyonge,si wa kuhusu safari yako, hapana!! Lengo ni kuelezea siku kumi  za msononeko wa moyo wangu kutokana na kauli tata na ya Hatari kwa Amani tuliyonayo tokea Uhuru.

Kauli hiyo tata ilitolewa na mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe uchaguzi mdogo Kinondoni.

Rais wetu mpendwa pamoja na siku hiyo Mbowe akihutubia kuwadharau watu wa Chato kijiji ulikozaliwa na kubwa akitumia maneno ya hovyo kwa Mkuu wa nchi, Rais na Amirijeshi Mkuu wa nchi lakini mbaya zaidi ni kauli mbaya, mbaya, mbaya sana kwa taifa na bado yuko uraiani.

KAULI YA MBOWE KUTAKA WATANZANIA TUFE
"Nitaongoza mapambano nchi hii, nitaongoza mapambano nchi hii, hata kama Watanzania 100 watakufa wataleta haki nchi hii, Lazima tukubali kubeba majeneza! Lazima tukubali nini. (MKUTANO UNAJIBU; kubeba majenezaa!!’) Ni wangapi wanasema tufanye kama Misri na Libya? Watakao kufa hata wakiwa 200 tuko tayari kwa mapambano na wao wanafikiri ni Kinondoni tu, lakini Ilala itawaka pia nchi nzima iwataka moto". Ni Maneno ya Freeman Mbowe Mbunge wa Hai, katika mkutano wa kufunga kampeni wa  16/02/2018 uliofanyika viwanja vya Buibui, Mwananyamala Komakoma).

Hii ni moja ya kauli mbaya sana kuwahi kuisikia kwa kiongozi wa upinzani nchini.

Lakini kuna wanaomsifia Mbowe kwa hili, watu hawangaiki kulinganisha uhusiano wa matukio yaliyojitokeza baada ya kauli hii.

Rais wetu mpendwa mpaka ninapoandika haya Freeman Mbowe anayetaka tufe, tupigane, na akijua fika tukipigana atakayeumia si yeye wala wanae woote aliowaza, Si Dudley, Si Dennis, Si Nicole wala nani kwenye familia yake kwa kuwa uwezo wa kutorokea nje upo.

Mbowe anajua fika watakaoumia na Kufa ni watoto wa walala hoi zaidi ya 85% ya watanzania nikiwemo mimi na Familia yangu ya PAVEA, Ndugu, jamaa na marafiki zangu.
akini Mbowe. DK.  Mashinji, Halima Mdee, John Mnyika nk hawa wanajua fika wako kwenye kundi la 5% ya watanzania wenye pesa nyingi wanaoishi kama Malaika,ambao ndo hawataki unayoyafanya kwa taifa letu.
Japo najua kuna 10% ya wapambe wao ambao wanashangilia wasichokijua na wanashiriki vitendo vya kuvuruga nchi lakini wakae wakijua wao nao waweza pata shida kama kundi la kwanza la 85%.

*Rais wetu mpendwa* Najua uko Chato ukijiandaa kurudi Dar es Salaam na najua njiani ukiwa unarudi Dar es Salaam kuna vitu utafanya sehemu nyingi za mikoa vya maendeleo yetu kama kawaida yao.

*Rais wetu mpendwa* najua utanisoma utasema kimoyomoyo *Yona* haya yote nayajua na yatafanyiwa kazi,lakini kuna ambalo ni muhimu kwenye waraka huu mfupi.

JAMBO LA MUHIMU LA RAIS WETU MPENDWA KUTAFAKARI NA KUCHUKUA HATUA KWA AJILI YA UONGOZI WAKE KUHUSIANA NA KAULI YA MBOWE*

*Rais wetu mpendwa* kauli ya *Mbowe* japo imeniumiza sana kwa siku hizi zoote lakini mbaya zaidi ni namna *Viongozi wetu woote wa dini,Asasi za kiraia,Mashirika ya nje yaliyo ndani,Balozi zoote,vyombo vya habari,Maadmin wa Magroup ya Watsap,wakuu wa mikoa,wakuu wa wilaya,viongozi wa majeshi yetu,Marais wastaafu,Mawaziri wakuu wastaafu,viongozi wa vyama vya siasa na wanafiki wachache wanaojiona wazalendo kwa taifa nk* walivyokalia kimyaa kauli ya ajabu ya *Mbowe* ya kutubebesha majeneza,japo walau Msajili wa vyama vya siasa amesema kitu.
Hapa ndo wakati nayatafakari najiuliza wafuatao kwa nini nao wamekaa kimyaa *wapi Edward Lowassa,wapi Zitto Zuberi Kabwe,Wapi Sheikh mkuu Aboubakary Zubeiry,wapi Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,wapi Kardinali Pengo nk*.

*Rais watu Mpendwa* tarehe 05/11/2015 ulipoenda kuapishwa maana yake ni wewe pekee ulipewa dhamana ya miili na mioyo yetu watanzania,yaani tukio lile la kuapishwa ulichukua dhamana ya watanzania woote,mingine ni Mihimili kukusaidia kuongoza nchi nasema viongozi wengine woote ni *CATALYST*.
Pointi yangu ni kuwa Nchi hii umepewa na watanzania peke yako,na ndo maana ukitoka madarakani utalaumiwa peke yako au utasifiwa peke yako,kwa hili jiridhishe kwa Marais waliopita kwenye lawama,au sifa,naomba ukipata muda walau *Unene kidogo*.

*KWA NINI NAWAZUNGUMZIA HAO NA KWA NINI NILITAKA WALAANI KAULI YA KIZANDIKI YA MBOWE?*

*Rais wetu mpendwa* Utakumbuka kuna baadhi ya viongozi wa Mshirika yasiyo ya kiserikali wamekuwa wakitoa kauli mara kwa mara ya kulaani na kukemea mambo ambayo mengine huwa ni ya uongo kabisa kisa waikomoe *CCM na uongozi wake*.
Lakini hao hao wanafiki wamepata kigugumizi kukemea kauli ya hovyo na ya ajabu kwa vile tu imesemwa na *Mwenye saccoss ya chadema*.

*Rais wetu mpendwa* Ukiwa Chato naomba utafakari sana,ujue hatua unazozichukua ni hatua muhimu kwa ajili ya wanyonge na ndo maana waliokuwa wapiga dili 5% na wapambe wao 10% wanapambana sana kuhakikisha unakata tamaa,nasema *Usikate tamaa uko njia sahihi* Songaa.

Mwisho, *Rais wetu Mpendwa* leo kwa mara ya kwanza tunashuhudia miradi mingi mikubwa inatekelezwa,na wakati mwingine tunakuhurumia.
Miradi kama ya *Reli ya Standard gauge,Flying over,Mradi wa kitakatifu wa Umeme wa uhakika Stigglers gorge nk* halafu tubebeshwe majeneza chaa!!!! *Mh.Rais wetu mpendwa Dr John Joseph Pombe Magufuli* walau *Nena kidogo*.

*Joseph Yona* Mtanzania.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Mdau, andikamaoni yako hapa yasaidie kujua wewe unafikiri nini kuhusu posti hii. Tafdhali, Maoni yako yasiwe ya uchochezi wa aina yoyote.. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

CCM Blog. Powered by Blogger.