LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 16, 2017

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONGOZA MAPOKEZI YA MAKAMU WA RAIS KUHAMIA MKOANI DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongaza viongozi na wananchi wa Mkoa wa Dodoma katika mapokezi rasmi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan baada ya kuhamia Mkoani Dodoma leo Desemba 15, 2017. kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa salamu za kumkaribisha Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan aliyehamia rasmi Mkoani Dodoma leo Desemba 15, 2017.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan wakiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Januari Makamba wakicheza ngoma ya Mwinamila wakati wa Makaribisho ya Makamu wa Rais Mkoani Dodoma leo Desemba 15, 2017.
Balozi Job Lusinde akitoa salamu za shukurani kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa Dodoma kwakuhamia Makamu wa Rais Mkoani Dodoma.

Na Beatrice Lyimo, MAELEZO-DODOMA

Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amehamia rasmi Makao Makuu ya Nchi Dodoma leo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli alililitoa tarehe 25, Ju.

 Akizungumza wakati wa halfa ya kumkaribisha, Makamu wa Rais amesema kuwa mpaka sasa ni mwaka mmoja na nusu tangu tamko la kuhamia Dodoma litolewe hivyo Serikali ipo na inatekeleza majukumu yake.

“Siku ya leo ilikuwa mawazoni mwangu, ninafurahi imefika na pia ninamshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa maandalizi mazuri ya kunipokea ” Alisisitiza Mhe. Samia

Aidha, Mhe. Samia amesema kuwa Ofisi yake imekuja na agenda ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani hivyo  wameandaa programu mbalimbali ikiwemo ya upandaji miti .

“Tarehe 21, Disemba mwaka huu kutakuwa na shughuli ya upandaji miti hivyo tunaomba wakazi wa mkoa wa Dodoma kutuunga mkono ili kuweza kutimiza azma hii” ameongeza Mhe. Samia.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa Baba wa Taifa aliweka nia ya Serikali kuhamia Dodoma tangu mwaka 1973 na leo Serikali ya Awamu ya Tano imetimiza ndoto hiyo.

“Tunaendelea kuamini kwamba tamko la Rais linatekelezeka ambapo mpaka sasa watumishi 2816 tayari wameshahamia Dodoma na wanaendelea kutoa huduma za Serikali na  kuanzia Februari mwaka 2018 tunaendelea kupokea watumishi wengine” amefafanua Waziri Mkuu.

Naye aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Pancras Ndejembi ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutimiza historia ya Mwalimu Nyerere ya Dodoma kuwa Makao Makuu.

“Sikuwaza kama kuna siku Makao Makuu yatakuwa Dodoma kwa sababu siku nyingi mambo haya yanazungumzwa sasa yamekamilika kwa vitendo, leo nina furaha sana kuona ndoto ya tangu mimi kijana imetimia” ameongeza Mzee Ndejembi.

Kwa upande wake Balozi Job Lusinde amesema kuwa “leo Makamu wa Rais anahamia Dodoma, kweli Mungu hupanga na Mungu huweka wakati wake, leo imekuwa”.

Mbali na hayo Balozi Job Lusinde amesema kuwa Makamu wa Rai amekuja kipindi ambacho Mkoa wa Dodoma unaanza kuandaa mashamba kwa ajili ya kulima, hivyo kumpatia jina la kabila hilo “Mbeleje” likimaanisha kipindi cha kuandaa mashamba.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages