LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 7, 2017

RAIS DK. MAGUFULI AFANYA MABADILIKO YA BARAZA LA MAWAZIRI, LEO

IKULU, DAR ES SALAAM
Rais Dk. John Magufuli leo Oktoba 07, 2017 amefanya mabadiliko ya Baraza lake la Mawaziri kwa kuongeza idadi ya Wizara, kuteua Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya na kuwahamisha Wizara baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu jijini Dar es Salaam, imesema, katika mabadiliko hayo Rais Magufuli ameongeza idadi ya Wizara na Mawaziri wake kutoka 19 hadi 21, na Naibu Mawaziri kutoka 16 hadi 21.

Ikulu imesema, iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini imegawanywa na sasa kuwepo Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini, na iliyokuwa Wizara Kilimo, Mifugo na Uvuvi imegawanywa na kuwepo Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Taarifa imeongeza kwamba, Rais Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa ametangaza mabadiliko hayo Ikulu Jijini Dar es Salaam na lifuatalo ni Baraza la Mawaziri kufuatia mabadiliko hayo.

1.    Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
I.    Waziri – George Huruma Mkuchika

2.    Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
I.    Waziri - Selemani Said Jafo
II.    Naibu Waziri - Joseph Sinkamba Kandege
III.    Naibu Wazri - George Joseph Kakunda

3.    Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
I.    Waziri - January Yusuf Makamba
II.    Naibu Waziri - Kangi Alphaxard Lugola

4.    Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu.
I.    Waziri - Jenista Joackim Mhagama
II.    Naibu Waziri - Anthony Peter Mavunde (Kazi, Vijana na Ajira)
III.    Naibu Waziri -Stella Alex Ikupa (Walemavu)
       
5.    Wizara ya Kilimo.
I.    Waziri - Dk. Charles John Tizeba
II.    Naibu Waziri - Dk. Mary Machuche Mwanjelwa

6.    Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
I.    Waziri - Luhaga Joelson Mpina
II.    Naibu Waziri - Abdallah Hamis Ulega

7.    Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
I.    Waziri - Prof. Makame Mbarawa Mnyaa
II.    Naibu Waziri - Mhandisi Atashasta Justus Nditiye
III.    Naibu Waziri - Elias John Kwandikwa

8.    Wizara ya Fedha na Mipango.
I.    Waziri - Dk. Philip Isdor Mpango
II.    Naibu Waziri - Dk. Ashatu Kijaji

9.    Wizara ya Nishati.
I.    Waziri - Dk. Medard Matogoro Kalemani
II.    Naibu Waziri - Subira Hamis Mgalu

10.    Wizara ya Madini.
I.    Waziri - Angellah Kairuki
II.    Naibu Waziri - Stanslaus Haroon Nyongo

11.    Wizara ya Katiba na Sheria.
I.    Waziri - Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi.


12.    Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
I.    Waziri - Dk. Augustine Philip Mahiga
II.    Naibu Waziri - Dk. Susan Alphonce Kolimba

13.    Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga (JKT).
I.    Waziri - Dk. Hussein Ali Mwinyi

14.    Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
I.    Waziri - Mwigulu Lameck Nchemba
II.    Naibu Waziri - Mhandisi Hamad Yusuf Masauni

15.    Wizara ya Maliasili na Utalii.
I.    Waziri - Dk. Hamisi Andrea Kigwangalla
II.    Naibu Waziri - Josephat Ngailonga Hasunga

16.    Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
I.    Waziri - William Vangimembe Lukuvi
II.    Naibu Waziri - Angelina Sylivester Mabula

17.     Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
I.    Waziri - Charles Paul Mwijage
II.    Naibu Waziri - Mhandisi Stella Martin Manyanya

18.     Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
I.    Waziri - Prof. Joyce Lazaro Ndalichako
II.    Naibu Waziri - William Tate Ole Nasha

19.  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
I.    Waziri - Ummy Ally Mwalimu
II.    Naibu Waziri - Dk. Faustine Engelbert Ndugulile

20.    Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
I.    Waziri - Dk. Harrison George Mwakyembe
II.    Naibu Waziri - Juliana Daniel Shonza

21. Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
I.    Waziri - Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe
II.   Naibu Waziri - Jumaa Hamidu Aweso

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Kaimu Karani wa Baraza la Mawaziri.Stephen Kagaigai kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuchukua nafasi ya Dk. Thomas D. Kashilila ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Taarifa hiyo ya Ikulu imesema, walioteuliwa wote wataapisha Jumatatu tarehe 09 Oktoba 09, 2017 saa tatu na nusu, asubuhi,  Ikulu Jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages