LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 21, 2017

CCM UBUGO WAMIMINA PONGEZI KWA RAIS DK.MAGUFULI, LEO

Tamko rasmi la CCM Wilaya ya Ubungo kumpongeza Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Magufuli ambalo lilisomwa na Katibu wa CCM wa wilaya hiyo Salum Kalli, kwenye mkutano wa kikazi wa Wenyeviti wa Mashina na viongozi wa CCM na Jumuia zake ulioitishwa na Mwenyekiti mpya wa CCM wa Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja, leo
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja akisalimia, baada ya kuwasili ukumbini kuzungumza Wenyeviti wa Mashina na viongozi wa CCM na Jumuiya zake katika wilaya hiyo, katika Ukumbi wa Hoja, Kimara jijini Dar es Salaam, leo. Kikao hicho ambacho kilikuwa cha kazi kilihudhuriwa pia na walioomba kugombea Udiwani kwa ajili ya uchaguzi wa marudio katika Kata ya Saranga wilayani humo.
 Katibu wa CCM Wilaya ya Ubungo Salum Kalli akiwasili ukumbini kwa ajili ya kikao hicho

 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja (Wanne kushoto) akiwa na viongozi wengine wa meza kuu baada ya kuwasili ukumbini kuzungumza Wenyeviti wa Mashina na viongozi wa CCM na Jumuia zake katika wilaya hiyo, katika Ukumbi wa Hoja, Kimara jijini Dar es Salaam, leo. Kikao hicho ambacho kilikuwa cha kazi kilihudhuriwa pia na walioomba kugombea Udiwani kwa ajili ya uchaguzi wa marudio katika Kata ya Saranga wilayani humo
 Baadhi ya viongozi wakicheza ukumbini nyimbo za shamrashamra kwenye mkutano huo
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja (kushoto) akicheza na mmoja wa wajumbea wa mkutano huo ambaye ana ulemavu wa mguu
 Mmoja wa walioomba kuwania Udiwani katika uchaguzi wa marudio kata ya Saranga Henry Chenya akisalimia wana CCM kwa hamasa wakati wa mkutano huo wa ndani
 Mmoja wa walioomba kuwania Udiwani katika uchaguzi wa marudio kata ya Saranga Mdoe Haroun akisalimia wana CCM kwa hamasa wakati wa mkutano huo wa ndani
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Wilaya ya Ubungo Justin Sambo (kulia) akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo Lucas mgonja wakati wakishauriana jambo kwenye mkutano huo wa ndani
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja akimsikiliza Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo Salum Kalli wakati wa mkutano huo
 Hekaheka ukumbini
 Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Ubungo Mbaraka Masudi akipiga push up wakati akichangamsha mkutano huo
 Mbaruku Masudi akizungumza baada ya kuhamasisha kwa push up kwenye mkutano huo
 Viongozi wakinyoosha mikono kukubali moja ya maelezo yaliyotolewa na viongozi wakuu kwenye mkutano huo
 Walioomba kugombea Udiwani katika Uchaguzi wa marudio Kata ya Saranga wakiinua mikono baada ya kutambulishwa
 Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Ubungo Mama Tindwa akitoa nasaha zake
  Katibu wa Siasa na Uenezi Kata ya Kibamba Clement Mgeto akisalimia baada ya kutambulishwa kwenye mkutano huo
 Mwenyekiti wa CCM Kata ya Saranga Iren Dafa akifungua mkutano huo
 Katibu wa CCM Kata ya Saranga Ramadhani Bagambele akizungumza wakati akimkaribisha Dafa
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Wilaya ya Ubungo Justin Sambo akizungumza kwenye mkutano huo
 Katibu wa CCM Wilaya ya Ubungo Salum Kalli akizungumza kwenye mkutano huo
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja  akihutubia na Wenyeviti wa Mashina na viongozi wa CCM na Jumuia zake katika wilaya hiyo, katika kikao cha kikazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoja, Kimara jijini Dar es Salaam, leo. Kikao hicho ambacho kilikuwa cha kazi kilihudhuriwa pia na walioomba kugombea Udiwani kwa ajili ya uchaguzi wa marudio katika Kata ya Saranga wilayani humo.
 Mwanasheria wa CCM Mwesigwa Zaid akiwapiga msasa wa sheria za uchaguzi waliohudhuria mkutano huo
 Wawakilishi kutoka kata zote za wilaya ya ubungo waliohudhuria mkutano huo
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja  akitoka ukumbini na baadhi ya viongozi baada ya mkutano huo.. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages