Wednesday, September 6, 2017

MWENYEKITI WA CCM KATA YA KIVUKONI SHARIK CHOUCHULE AJITOLEA DAMU KUUNGA MKONO VIJANA

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kivukoni, Sharik Choughule, mwishoni mwa wiki aliwaunga mkono vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM, kwa kushiriki kujitolea damu katika kambi iliyofanyika Chanika, wilayani Ilala, Dar es Salaam, kwa ajili ya kusaidia damu kina mama na watoto.

Choughule akichangia alisema, ameamua kuchangia damu kwa sababu anafahamu umuhimu wa mahitaji ya damu kwa wagonjwa hasa kina mama na watoto.

"Nawapongeza Vijana wa UVCCM kwa kuamua kufanya zoezi hili la utoaji damu kwa ajili ya kina mama na watoto, hii ni hatua ya kizalendo ambayo inapaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania", alisema Choughule.

Alisema, vilevile aliamua kuwenda kujitolea damu kwa sababu anatambua kuwa vijana ndiyo nguzo ya Chama Cha Mapinduzi hivyo ni lazima kuungwa mkono kila wanapofanya jambo jema kwa taifa.
 Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kivukoni, Sharik Choughule aqkionyesha damu aliyojitolea katika kambi hiyo. Chini ni picha mbalimbali wakati akijitolea damu katika zoezi hilo
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

CCM Blog. Powered by Blogger.