LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 8, 2017

WAZIRI MASAUNI ONGOZA MATEMBEZI YA SIKU YA MABALOZI WA USALAMA BARABARANI MKOANI DODOMA, LEO

 Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani, Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiongoza matembezi ya Mabalozi wa Usalama Barabarani kuingia katika Uwanja wa Mashujaa, kuadhimisha siku yao iliyofanyika Kitaifa leo mkoani Dodoma leo. Kulia ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo,Mkuu wa  Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi Mohamed Mpinga
 Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani, Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani ambapo aliwaasa madereva kufuata sheria kupunguza tatizo la ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikisababisha vifo na kuacha idadi kubwa ya vifo na majeruhi. Wapili kushoto ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Mkuu wa  Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,Kamishna Msaidizi wa Polisi Mohamed Mpinga na anayefuatia ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa. Maadhimisho hayo yamefanyika Kitaifa leo katika Uwanja wa Mashujaa,leo mkoani Dodoma.

 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mkuu wa  Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi Mohamed Mpinga, akizungumza wakati wa maadhimisho hayo. Kulia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani, Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na kulia ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa.
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa akizungumza wakati wa Maadhimisho hayo.

 Mabalozi wa Usalama wa Barabarani wakiwa kwenye maadhimisho hayo
 Msanii Faustine Matina ambae ni Balozi wa Usalama Barabarani, akiimba wimbo wa kuhimiza masuala ya kuzingatia sheria za usalama barabarani wakati wa maadhimisho hayo.
 Muathiwa wa ajali anayefahamika kwa jina la Mpemba Asilia, akizungumza na Mabalozi wa Usalama Barabarani, alipofika katika maadhimisho hayo
Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani, Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(watano kulia), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mabalozi wa Usalama Barabarani wakati wa  Maadhimisho hayo. Wasita kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mkuu wa  Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Mohamed Mpinga. PICHA: WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages