LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 31, 2017

WAKUU WA VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII WAHI,IZWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU KATIKA UTENDAJI KAZI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga(kushoto) akijadiliana jambo na Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare ambaye ni mwenyekiti wa mafunzo Bw. Paschal Mahinyika(kulia) wakati wa mafunzo ya ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji kwa wakuu wa Vyuo vya maendeleo ya Jamii yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017.

Na Erasto Ching’oro WAMJW

Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) Bibi. Sihaba Nkinga amewahimiza Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii, kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika utendaji wao wa kazi katika kuendesha vyuo wanavyovisimamia.


Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao  kuhusu udhibiti wa viashiria hatarishi vya utendaji na utawala ikiwa ni pamoja na  kuzingatia nidhamu ya matumizi ya fedha katika utendaji wao wakazi wa kila siku ili kuepuka hoja za ukaguzi wa fedha.


Amesisitiza kuwa wakuu wa vyuo ni watumishi wa Umma na wanapaswa kuzingatia weledi mahala pa kazi kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu zote za utumishi wa Umma katika kutimiza majukumu yao.


“Niwatake Wakuu wa Vyuo mliopo hapa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo katika kundesha vyuo mnavyoviongoza tuondokane na dosari katika suala la udhibiti wa Fedha katika matumizi” alisema Bibi Sihaba.



Aidha, Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga, amesema kuwa mara baada ya mafunzo haya maalum, Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini vitaweza kufuta hoja zote za ukaguzi mahala pa kazi kutokana na kufanya kazi kwa kufuata maadili, maarifa na miongozo na weledi unaotakiwa katika uendeshaji wa vyuo.


Aidha Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga amewataka wakuu wa vyuo kuongeza umakini katika utekelezaji wa majukumu yao mahala pa kazi, kuimarisha mawasiliano katika uwajibikaji wa pamoja kwa kuimarisha mifumo ya utendaji kazi katika vyuo vya maendeleo ya jamii.


Mafunzo haya yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) na kushirikisha vyuo vya Buhare, Uyole, Rungemba, Ruaha, Mabughai, Monduli na Mlale
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati waliokaa)akiwa akiwa na wakufunzi wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini wakati wa mafunzo ya udhibiti wa viashiria hatarishi mahala pa kazi yaliyofanyikakatika Ukumbi wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo leo 31.7.2017.
  Picha na Erasto Ching’oro WAMJW

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages