LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 28, 2017

TANZANIA KUENDELEZA USHIRIKIANO NA INDIA KATIKA NYANJA MBALIMBALI

Waziri Mkuu akiwa na Mkuu wa Majeshi wa India
DAR ES SALAAM
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania itaendeleza ushirikiano na Serikali ya India katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya ulinzi.

Ametoa kauli hiyo leo, Julai 28 , 2017 alipofanya mazungumzo na Mkuu wa Majeshi wa India, Admiral Sunil Lanba jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema Tanzania na India ni nchini ambazo zina uhusiano mzuri na wa muda mrefu, ambapo ameahidi kwamba Serikali itaendelea kuudumisha.

 “Ushirikiano wa Tanzania na India ni wa kihistoria, hivyo tutauendeleza na kuudumisha. India tunashrikiana nao katika sekta za uchumi, afya, elimu na ulinzi.”

Waziri Mkuu ameishukuru Serikali ya India kwa ufadhili walioutoa kwa Tanzania  katika kuimarisha miradi ya maji kwenye mikoa mbalimbali nchini.

Pia Waziri Mkuu amewakaribisha raia wa India kuja kutembelea maeneo ya  utalii nchini ukiwemo mlima wa Kilimanjaro, mbuga za wanyama na visiwa vya Zanzibar.

Kwa upande wake, Mkuu wa Majeshi wa India, Bw. Lanba ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano inaoutoa kwa Serikali ya India hususan katika masuala ya ulinzi.

Amesema wamefanya kikao na Mkuu wa Majeshi nchini Generali Venance Mabeyo ambapo katika mazungumzo yao wameweka mikakati ya kushirikiana katika kuimarisha ulinzi hususan maeneo ya mipakani pamoja na masuala ya mafunzo. PICHA/>BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages