Tuesday, July 25, 2017

SIMULIZI KUTOKA MKOANI KILIMANJARO

Jana nikiwa katika matembezi binafsi katika mteremko wa mlima kilimanjaro jirani na Wilaya ya Arumeru nilikutana na wadada wadogo na wanguvu wawili mmoja akiitwa Regina na Mwingine Asteria walikuwa na furaha na tabasamu tulipo onana na nikavutwa kuwauliza maswali kadhaa ikiwemo wakiwa wakubwa watapenda kufanya kazi gani. Regina alisema atapenda kuwa Daktari na Asteria  alisema atapenda kuwa Mwalimu.
Wakati tunaonana walikuwa wakirejea nyumbani basi na mimi nikashiriki kusaidia mojawapo ya mzigo na safari ya kuelekea kwao ndipo ilipoanza.
Nimejifunza mengi kwa wasichana hawa wadogo na wanguvu, wanasoma bure shule ya msingi na wazazi wao hawahojiwi ada tena, wana ndoto kubwa maishani mwao ambayo kwa kujiamini kabisa wameniahidi kuitimiza.
Mpaka natua mzigo kwao sikuwa nimewaeleza natoka wapi, lakini, kama msimamizi wa sera na Ilani ya CCM nitahakikisha uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake unaendelea kutekeleza ahadi zake kwa watanzania na hasa katika eneo la elimu ambalo kwa kupeleka bilioni 18 kila mwezi, Regina na rafiki yake wanasoma bure na watasoma bure mpaka sekondari na tutahakikisha wanafika Chuo Kikuu ili baadaye watimize ndoto zao na kuwa raia wema wanaoijenga nchi yao Tanzania.
H.H. Polepole
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi (CCM)
Kilimanjaro
Julai 24, 2017
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.