LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 21, 2017

SHAKA AWATAKA VIJANA KUJIUNGA NA UJASIRIAMALI KIGOMA

 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kibondo Salome lihungilanywa akimkaribisha Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijna wa CCM, (UVCCM), Shaka Hamdu shaka wakati wa kusain kitabu cha Mahudhurio ya wageni wilayani kibondo.
 KAIMU Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijna wa CCM, (UVCCM), Shaka Hamdu shaka (wa pili kulia), akiwa katika mradi wa ufugaji samaki kwenye Kijiji cha Ming'inya wilayani Kibondo mkao wa Kigoma, juzi. Kuhoto ni Mbunge wa Viti Malumu, Zainb Katimba (CCM). Picha zote na Fahadi Siraji-UVCCM)
 Mhe Mbunge wa Viti Maalum Vijana Zainab Katimba akitoa  mchango wa fedha katika kikundi cha kinamama katika kijiji cha minyinya wilaya ya kibondo mkoani  kigoma.
  Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijna wa CCM, (UVCCM), Shaka Hamdu shaka akishiriki Kulima  katika shamba  la kikundi cha wajasiriamali wanawake katika Kijiji cha Kumhasha Kata ya Murungu, Kibondo.

Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijna wa CCM, (UVCCM), Shaka Hamdu shaka akishiriki upandaji mbogamboga katika shamba shamba la kikundi cha wajasiriamali wanawake katika Kijiji cha Kumhasha Kata ya Murungu, Kibondo.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijna wa CCM, (UVCCM), Shaka Hamdu shaka wa pili kulia akizungumza na kikundi cha wajasiriamali wanawake katika Kijiji cha Kumhasha Kata ya Murungu, Kibondo.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijna wa CCM, (UVCCM), Shaka Hamdu shaka akikagua kikundi cha Ujasilia mali cha mafundi wenyeulemavu katika Kijiji cha Kumhasha Kata ya Murungu, Kibondo.

Mbunge wa Viti Malumu, Zainabu Katimba (Kulia) akishiriki Kulima  katika shamba  la kikundi cha wajasiriamali wanawake katika Kijiji cha Kumhasha Kata ya Murungu,  wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma.
..........................................................................................................


Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Umoja wa Viijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM ) umesema vijana wanaoendelea  kulalamika bila kufanya kazi, kujituma na kutoa jasho la uchapakazi watakawia sana kufikia malengo chanya na kujikwamua hatimaye  maisha.

Hayo yameelezwa jana kaimu katibu mkuu shaka Hamdu Shaka alipotembelea kikundi cha ujasiriamali katika kata ya Mwandiga wilaya ya Kigoma vijijini Mkoani hapa .

Shaka alisema hakuna njia mbadala na ya mkato ya kujikwamua kimaisha na hali ngumu yoyote ya umasikini bila kijana mwenyewe kuamua kujishughulisha na kuzalisha mali hatimaye kujitegemea.
Aliwasifu wana kikundi hicho kwa kujikusanya, kupanga mipango na mikakati ya  mradi wa kufyatua matofali, kuzalisha sabuni na kuwa na kikundi cha Vicoba kwa mtimdo wa kuweka na kukopa pia kununu hisa.

"Vijana wengi huwa wanawaza, wanapanga na kutaka kutenda  hawatendi, kikundi hiki ni makini na kimeamua kuonyesha kwa vitendo jinsi kilivyopania kujikwamua na umasikini wa vipato hatimaye kujijenga kiuchumi "Alisema Shaka .

Shaka aliwahimiza watendaji wa halmashauri ya Kigoma vijijini kuona haja ya kukipa umuhimu kikundi hicho kwa kuwapatia wataalam, mitaji na vyanzo vya fedha. 

"Vijana mnakawia, jiungeni ili kushiriki katika shughuli za ujasiriamli kwa lengo la kuacha utegemezi badala yake mjiajiri na kujitegemea kiuchumi kama kikundi cha "Alisema 
Kaimu Katibu Mkuu pia alizindua kazi za uchimbaji wa mitaro kwa akili ya usambazaji wa maji safi na salama katika kata ya kalinzi na  kutazama maendeleo ya mradi wa ujenzi wa tangi la maji hatimaye akazumgumza na wanachama katika kikao cha ndani katika kata Mgaraganza  mkoani hapa .

Kwa upande wake Mbunge wa vijana Mkoa Kigoma Zainab Katimba ameahidi kukisaidia kikundi hicho kwa kuwapatia vyerehani vitano ili kuongeza mradi mwingine wa ushonaji kwa kina dada wa kikundi hicho. 
Aliwaeleza vijana hao waendelee na shime hiyo ya kujitolea na kutumia nguvu zao ili kufikia malengo yao ya kujijenga kiuchumi na kupata maisha bora. 

"Ingelikuwa vijana wote kigoma na Tanzania wanapitisha maamuzi mazito kama kikundi hiki, nchi yetu isingekuwa na vijana wanaolalamika, wanaosaka ajira au kulalamikia umasikini "Alisema Zainab. 
Hata hivyo Mbunge huyo alisema atafanya kila linalowezekana kuhakikisha vijana hao halmshauri ya Kigoma vijijini inawafuatilia na kuwatazama kwa macho mawili makoni vijana hao. 
End

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages