Monday, July 24, 2017

PROF.LIPUMBA AWAVUA UANACHAMA WABUNGE WANANE NA MADIWANI WAWILI CUF

Mweneyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba 

akizungumza na Waandishi wa Habari jana, 
jijini Dar es Salaam
DAR S SALAAM
Baraza Kuu la Uongozi la CUF limewafukuza uanachama wabunge wanane wa viti maalum na madiwani wawili pia wa viti maalum.

Miongoni mwa Wabunge hao wanane, ni pamoja na Kiongozi wa Wabunge wa CUF Riziki Shahali.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba wakati akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam.

Amesema wabunge na madiwani hao wamevuliwa uanachama wao kutokana na kukaidi wito waliopewa na Kamati ya Maadili na Nidhamu ya chama hicho juu ya tuhuma zinazowakabili ikiwemo kuhusishwa na vitendo ya usaliti ndani ya chama.

Aidha Prof. Lipumba amesema tayari wamemwandikia barua Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Job Ndugai juu ya maamuzi ya kuwafutia uanachama wabunge na madiwani hao.
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.