Saturday, July 15, 2017

NAIBU WAZIRI JAFO AHIMIZA WAAJIRI KUWASILISHA MICHANGO YA WANACHAMA KWA WAKATI

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akikabidhiwa fomu ya kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia Mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS), kutoka kwa Mfkurugenzi wa Uendeshaji, Bi. Neema Muro, (kulia), baada ya kufungua semina ya Mafunzo kwa wastaafu watarajiwa mkoni Dodoma Julai 14, 2017.
NA K-VIS BLOG, DODOMA


NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, Mhe. Selemani Jafo amejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia Mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS) na kuhimiza na kjtoa wito kwa waajiri wote nchini kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao katika mifuko ya hifadhi ya jamii kwa wakati kama sheria inavyowataka ili kuepuka usumbufu kwa wanachama wakati wa kupata Mafao yao wanapostaafu. 

Mhe. Jafo aliyasema hayo wakati akifungua semina ya mafunzo kwa wastaafu watarajiwa mkoani Dodoma Julai 14, 2017.Semina hiyo imelenga kuwajengea uwezo wastaafu hao watajiwa ili kuweza kufanya shughuli za ujasiriamali wakati muda wao wa utumishi wa umma utakapokoma.

Mhe. Jafo amewanyooshe kidole waajiri wenye tabia ya kutopeleka michango ya wanachama katika mifuko yao kitendo ambacho kinasababisha kero kubwa pindi watumishi hao wanapostaafu na kuanza kuhangaikia Mafao yao kutokana na taarifa za uwasilishaji michango katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kutokamilika.

“Nitoe rai kwa ndugu zangu watumishi wa umma ambao katika kipindi cha miaka miwili ijayo mtaondoka kwenye utumishi wa umma, yatumieni vema mafunzo haya ili mtakapopata mafao yenu basi tayari mtakuwa na nyenzo ya kuwasaidia kutumia vema fedha mtakazopata kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo, lakini pia kilimo na ufugaji wa kisasa na hatimaye kuyafanya maisha yenu kuwa bora baada ya utumishi wa umma.” Aiasa Mhe. Jafo.

Katika hatua nyingine, wimbi la viongozi kujiunga na Mpango wa uchangiaji wa Hiari yaani PSPF Supplementary Scheme, (PSS), Mhe. Jafo naye amejiunga na mpango huo na kuwahamasisha wastaafu hao watarajiwa na wananchi wengine kujiunga na Mpango huo kwani utawawezesha kuwa na hakikisho la kuweka fedha zao ili ziwasaidie kwenye miradi wanayotarajia kuibuni, ikiwa ni pamoja na kujipatia bima ya afya.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu, amebainisha kuwa mfuko huo unatarajia kulipa jumla ya Sh.Trilioni 1.3 katika kipindi cha 2017/18 ambazo ni Mafao ya watumishi 9,552 wanaojiandaa kustaafu katika kipindi cha kati ya Mwaka huu wa 2017 na mwaka ujao wa 2018.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, akitoa hotuba yake. "Mfuko umetenga kiasi cha shilingui Bilioni 1.3 kwa ajili ya kulipa mafao watumishi 9,552 wanaotarajiwa kustaafu kati ya mwaka huu wa 2017/2018."
Naibu Waziri Jafo akitoa hotuba yake.
Washiriki wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo.
Mzee mstaafu akitoa ushuhuda kwa kundi la wanachama wa Mfuko wa PSPF wanaotarajiwa kustaafu katika semina iliyoandaliwa na mfuko huo mkoani Dodoma.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.