LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 1, 2017

MAWAKILI WA KUZINGATIA SHERIA ZA NCHI NA ZA KIMATAIFA

NA   LIDYA CHURI  - MAHAKAMA YA TANZANIA
Kaimu Jaji Mkuu  wa  Tanzania,  Mhe. Profesa Ibrahim  Juma, amewataka  mawakili  kufanya kazi kwa kuangalia sheria za nchi  na za kimataifa ili kuweza kuwasaidia  Watanzania katika   masuala  yanayohusu sheria  hususan  wananchi wanyonge ili nchi ya Tanzania  iweze kufikia malengo ya kimaendeleo .

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Jaji Mkuu huyo, wakati hafla fupi ya  kuwapokea na mawakili wapya 248 walioapishwa na kukubaliwa kuwa mawakili, iliyofanyika leo  kwenye Kiwanja cha Mahakama  Kuu kilichopo jijini Dar es Salaam.

“Leo tumewaapisha mawakili  waliokubaliwa, nilifanya  nao mazungumzo kila mmoja, wengi wao ni vijana wadogo wenye miaka  25 hadi 30  ya  kufanya kazi ya sheria. Hivyo  kukubaliwa kwao  sio mwisho wa kusoma wanapaswa  kusoma  sheria za kimataifa ili kufahamu  sheria za utaratibu wan chi zingine,”

 Profesa Juma aliwataka  mawakili hao, hao waendelee kufanya kazi kwa weledi, kuzingatia maadili  na kuepuka kujiingiza katika vitendo vya rushwa,kwa sababu     bado wananchi  wana   hisia  kwamba  tatizo la rushwa  ni kubwa  ndani ya Mahakama  ya Tanzania.

“Wazazi na Serikali imetumia  gharama  kubwa  kuwasomesha,  hivyo watambue watambue mchango huu,  waisaidie  serikali  na wazazi wao ili  Tanzania  isonge mbele, alisisitiza Lidya Churi.

 Akijibu  swali lililoulizwa na  baadhi ya waandishi kuhusu kuwepo kwa tetezi kwamba  Chama cha Wanasheria  Tanganyika(TLS),  alisema sheria  ikitungwa haitalenga  mtu wala taasisi, hivyo  hofu hiyo haina sababu  kuwepo  kwa kuwa mawakili ni sehemu ya mahakama.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages