Thursday, July 27, 2017

KILIO CHA CHADEMA NI FEKI

Mwandishi Augustino Chiwinga
NA AUGUSTINO CHIWINGA
Siku za hivi karibuni chama cha demokrasia na maendeleo kimepata   na kinaendelea kupata mtikisiko mkubwa  baada wimbi la kukimbiwa na viongozi na wanachama wake kuongezeka.

Hali hiyo imeishtua hadi kamati kuu ya chama hicho ambapo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe alinukuliwa akisema kwamba Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kinanunua madiwani na wanachama wao ili wajiunge na CCM.

Ajabu iliyoje CCM iwe na fedha  nyingi kiasi  hicho za kununua madiwani wote hao na wanachama zaidi ya 10,000 wa chadema.

Ukweli ni kwamba CCM haifanyi siasa za kununua mtu , wimbi la madiwani na wanachama kutoka chadema wanaohamia CCM kwa kasi ni kielelezo cha mafanikio ya mageuzi makubwa iliyoyafanya CCM  ilipotimiza miaka 40  maarufu kwa jina la CCM MPYA.

Wale wanoahama chadema ni watu ambao  waliamini  kwamba Tanzania inahitaji uongozi mpya utakaofanya mapinduzi makubwa katika kila sekta hapa nchini.

Baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani , alianza kuonesha mwelekeo wa kujenga taifa jipya kabisa kwa kutumbua  mafisadi, kupambana na ubadhirifu  wa mali za umma  kutoa elimu bure kuboresha sekta ya afya, miundombinu na usafirishaji na kuhimiza uchapakazi  nk. .

Waliamini kwamba  uongozi wa juu wa chadema utaungana  na Rais Magufuli katika kulistawisha taifa hili kwa sababu pale mwanzoni walisema kwamba Rais Magufuli anatekeleza ilani ya UKAWA , lakini  badala yake wakamgeuka na kuanza kumpinga kwa kila kitu anachokifanya Mh. Magufuli.

Wapo  madiwani walioambiwa ni marufuku kushirikiana na wateule wa Rais kama vile wakuu wa mikoa , wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa Halmshauri.

Kiukweli hawakuelewa kwa nini wanapigwa marufuku hizo ilihali maendeleo katika Kata zao zinahitaji ushirikiano mkubwa baina yao madiwani na wateule hao wa Rais.

Lakini baadae walikuja kunga'mua kwamba wenzao waliodhani wanafanya siasa safi  zenye kuleta tija na maendeleo hawana dhamira hiyo bali wana ajenda zao nyingine za siri  zilizojificha .

Baada ya kuubaini ubabaishaji huo wa viongozi wa juu wa chadema ndipo walipoamua kukihama chama hicho na kujiunga na CCM.

Hivyo chadema katika hili waachane na dhana potofu kwamba CCM inawanunua madiwani, ni ubabaishaji wao wenyewe ndio unaowapelekea wakimbiwe  na madiwani wengi kila kukicha.

Pili hakuna haja ya kuwatuhumu kwamba wamenunuliwa kwa sababu Tanzania ni nchi ya kidemokrasi kila raia anaruhusiwa kujiunga na chama  cha siasa akipendacho, hivyo chadema isiwafunge speed governor madiwani na wabunge  wake wanaotaka kuhamia CCM.

Chadema haijawawekea gundi au kuingia mkataba na viongozi wao kwamba hawaruhusiwi kuhama chadema.
Pia itambulike chadema sio chama bora kuzidi CCM kwa namna yoyote na kwa vile kimeshindwa kukidhi matarajio ya viongozi hao basi tutegeme madiwani wengi zaidi na wabunge  watakaokimbia chama hicho.

Najua kinachowaumiza kichwa chadema ni kwa sababu mtikisiko huu wa kukimbiwa na na madiwani unatokea kanda ya kaskazini ambako ndipo wanapojinasibu kwamba ni ngome yao kubwa lakini napenda kuwakumbusha kwamba mwiba huingilia ulipotokea chadema ilianzia kaskazini na hata kufa pia inaanzia kufia huko huko kaskazini kabla ya moto huo kusambaa katika mikoa mingine hapa nchini.

Waswahili wana msemo wao maarufu kwamba huwezi kumjua mchawi kama na wewe sio mchawi, hivyo kwa vile chadema wanasema CCM inanunua madiwani watuambie basi na wao basi Sumaye Kingunge na Lowassa waliwanunua kwa shillingi ngapi, la sivyo kilio chao cha  kwamba  madiwani wananunuliwa ni feki  ni kisingizo tu wanachokitumia  katika kuficha madhaifu makubwa ya chama chao.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.