Sunday, July 9, 2017

DC MTATURU ASHIRIKI MAZOEZI NA WANANCHI YA PUMA LEO

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu leo asubuhi ameshiriki mazoezi pamoja na wananchi wa Kata ya Puma wilayani humo lengo likiwa ni kuunga mkono maelekezo ya makamu wa Rais Samiah Suluhu Hassan ya kufanya mazoezi kila jumamosi ya pili ya kila mwezi.

Akiwa katika mazoezi hayo msisitizo wake mkubwa kwa wananchi ni kujenga utaratibu wa kufanya mazoezi ili kuweza kuondokana na magonjwa yasiyo ya kuambikiza na kuufanya mwili kuwa imara katika utendaji wao wa kazi.

Aidha amewataka kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara kwa kuwa uchumi wa Taifa unajengwa kwa wananchi kuwa imara kiafya.

Mbali na kufanya mazoezi hayo amekabidhi mpira wa miguu kwa ajili ya timu ya walimu ya wilaya lengo likiwa ni kujenga ari kwa wananchi kupenda michezo na hivyo kuweza kuinua kiwango cha soka wilayani humo
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.