Friday, July 7, 2017

BAADHI MAMBO 20 YANAYOMFANYA DK. JOHN MAGUFULI KUWA WA KIPEKEE

Mwenyekiti wa CCM Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli (Pichani), hata kabla ya kuwa Rais alionyesha kuwa ni mtu wa kipekee, kwa namna ya uwezo wake wa kibinadamu katika kuyaelewa mambo mbalimbali kwa haraka na njia za kuyapatia ufumbuzi kwa haraka.
Bila kumlinganisha na yeyote, Mtayarishaji Mkuu wa CCM Blog, Bashir Nkoromo, amebahatika kupata dondoo hizi zenye mambo 20 ambayo ni baadhi ya yanamfanya Dk. Magufuli kuwa mtu wa kipekee na hivyo kuona kwamba ni vizuri na tija kuweka hapa ili nanyi wadau wa Blog hii mzisome. Sasa endelea..
-----------------------------------------------
Rais1. Magufuli ameandikwa kwa lugha 134 kwa mwaka jana katika nchi mbali mbali duniani.

2. Magufuli ana uwezo mkubwa wa kukariri namba hadi 22, kwa wakati mmoja, craming capacity yake iko 89% , wakati kitaalam normal craming capacity ya binadamu ni 62%

3. Magufuli aliwahi kuanguka na helicopter akiwa na Said Meck Sadik wakati wakikagua uharibifu uliofanywa na mvua mkoani Dar es Salaam,

4. Jakaya Kikwete akiwa Rais, na Pinda akiwa Waziri Mkuu walikuwa wanatupiana mpira nani am-face Magufuli wakati wa kutengua baadhi ya maamuzi yake katika wizara ya ujenzi, ilibidi Pinda aahirishe safari yake ya Kagera alipofanya ziara kwa mambo ya sukari kwanza akaja wakutane na Kikwete kujadili wanamuanzaje Magufuli kumueleza asibomoe jengo la TANESCO Ubungo

5. Magufuli alikuwa anamsapot sana Dk. Slaa na upinzani wa maana hasa wa Kafulila, alikuwa anampa vimemo kafulila akomae na Escrow ambayo ilionekana ni ya utapeli,

6. Magufuli aliwahi kwenda Minaki high school kumwadhibu kijana wake aliyetaka kuhama kinyemela kwakuwa alikuwa anataka shule nyinginezo siziso za serikali, akipanga njama na mama yake, lakin Magufuli alikataa kata kata, akasema mwanangu atasoma hapa hapa kama wa wengine,

7. Magufuli ana nguvu ya ajabu Na ya ziada, hasa kwa wale ambao walitaka kumkwamisha mara nyingi anagundua njia hizo hata za kishirikina, mfano Morogoro kwenye mikutano na watu wa TANROADS alikataa kukalia kiti ambacho alitengewa, Na baada ya mtu mwingine kukikalia ikawa madhara, maana alilengwa yeye akiwa Waziri wa Ujenzi,

8. Magufuli Na marafiki zake wamekuwa maadui kisa anasimamia ukweli , umefika mda mpaka ndugu zake wa ukoo hawampendi sana maana walidhani Akiwa serikalini atawapa ulaji, Jambo ambalo Magufuli hakubaliani nalo kabisa,

9. Magufuli aliwahi kuangusha nyumba ya baba Mdogo yake, ambaye alijenga barabarani, hakujali kuwa ni ya baba Mdogo

10. Magufuli kapanda ndege za kwenda nje ya nchi Mara 7 tu tokea amekuwa serikalini
Moja ilikuwa Libya, nyingine ulaya, Na nyingine Japan,
Tokea amekuwa rais amepanda ndege 3 tu za kwenda nje, yaan Kenya , Uganda na Ethiopia ,Rwanda alienda kwa gari,

11. Magufuli ni Rais maskini kuliko marais wote Africa, ikumbukwe rais tajiri ni wa Angola bwana Dos Santos,

12. Magufuli Hana usafiri wa gari anatumia usafiri wa serikali, Na magari aliyekuwa anapewa Akiwa mbunge alikuwa anayakabidhi katika taasisi mbali mbali,

13. Magufuli ni rais aliyevunja record ya kutembea mwendo mrefu kwa gari Akiwa rais , km 670, lakin ikumbukwe Nyerere alivunja rekodi ya kutembea kwa miguu kutoka Butiama hadi Mwanza kwa wiki kadhaa na aliyepewa jukumu la mapokezi na kujenga mahema alikuwa Mzee Kikwete akiwa Jeshini,

14. Magufuli ni rais ambaye amevunja rekodi ya kutamaniwa Na nchi nyingi dunian kuwa mtawala wao, Kama, Egypt, Australia, Nigeria, Ghana, Mozambique, Uganda, Kenya , South Africa, Bolivia, Columbia, Madagascar, Nepal, Thailand, Angola, Na nyinginezo,

15. Magufuli Akiwa mbunge aliwahi kukataliwa kupitishwa kwenye kura za maoni mwaka 1995 ikiwa ni jimbo la chato biharamulo, vijana waliandamana Na kufunga vikufuri vidogo kwenye ruksi wakimaanisha wanamtaka Magufuli, ikabidi uchaguzi wa kura za maoni urudiwe, akapita,

16.Magufuli anapenda sana story yuko radhi audhulie sehem Zake alizozoea kupata story hata kama ni Rais.

17. Magufuli ni shabiki wa timu ya yanga, kwa vilabu dunian anapenda sana Arsenal, Na kwa Hispania anapenda Barcelona, Ila kwa timu za taifa anapenda sana taifa stars, pili Brazil.

18. Mheshimiwa Magufuli anapenda mziki wa zaman Na wa kisasa yaan bongofleva, Na msanii anayempenda sana ni darasa Na Mwana FA.

19 mheshimiwa Magufuli amekataa mialiko 17 toka nchi mbali mbali dunian , ikiwemo USA.

20. Ni rais anayependa sana kutumia lugha yake ya taifa hata Akiwa nje
NI JASIRI WA AJABU SANA
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.