LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 7, 2017

WAZIRI MKUU KATIKA HAFLA YA UZINDUZI NA UGAWAJI NA USAMBAZAJI WA VIFAA KWA WANAFUNZI WENYE UHITAJI MAALUMU

Waziri Mkuu akisalimiana na viongozi mbalimbali wakati alipowasili katika  Shule ya Msingi ya Uhuru Mchanganyiko Dar es Salaam jana 



 Mshereheshaji akiongoza uzinduzi huo
 Katibu Tawala wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo (kulia) akizungumza jambo na maofisa wa Jeshi la Magereza kabla ya kuwazili mgeni rasmi
 Afisa Elimu Ilala, Elizabeth Thomas (kulia) akiwaunga mkono wanafunzi hao kwakutoa burudani kwa kucheza nao

 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Umoja iliyopo Yombo Kiwalani ikitumbuiza wimbo wa Makirikiri katika uzinduzi huo, ambapo Waziri, Ndalichako ametowa ofa wafike Dodoma kuendeleza kutowa huduma hiyo katika sherehe zinazo tarajiwa kufanyika mjini humo hivi karibuni
  Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako akihutubia  katika uzinduzi huo
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akitowa salam za mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati wa uzinduzi na ugawaji na  usambaza wa vifaa  kwa wanafunzi wenye uhitaji maalum  Nchi nzima uzinduzi uliyofanyika Dar es Salaam jana,  ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa 
 Wanahabari wakiwa kazini

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia wakati wa uzinduzi huo,  ambapo alianza kuwashukuru walimu na kuwasihi kwa namna wanavyo shirikana ilikuweza kulifikisha gurudumu la Elimu mahala tunapohitaji lifike,

Hayo aliyasema jana Jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa vifaa maalumu kwa wanafunzi wenye mahitaji hayo ambapo alisisitiza na kuwashukuru waandaaji na kumpa heshima ya kumualika kuwa mgeni rasmi.

Aidha kipekee kabisa nishukuru Shirika la Lanes lililoshirikiana na Serikali yetu kusaidia upatikanaji wa vifaa hivi ambapo punde nitazindua na kufikabidhi ugawaji wa vifaa hivi.

Kwaniaba ya Serikali napenda kuwaahidi kwamba vifaa hivi vitatumika kama vilivyo kusudiwana vitawafikia walengwa wote tayari kwa matumizi

Ndugu wananchi, Walimu na Wanafunzi, nitazindua zoezi la usambazaji vifaa kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu kwa mikoa yote 26 ya Tanzania Bara 

Zoezi la hili hapa lilitanguliwa na zoezi la usambazaji wa vifaa vya masomo ya Sayansi, kwenye Sekondari, tulifanya Lugalo kwa hiyo  ni siku ya Elimu na sasa tumefika hapa katika Shule ya Msingi ambapo tutahitimisha zoezi hili 

Zoezi hili litanufaisha shule za Msingi 213 kati ya shule 408 na shule za Sekondari 22 kati ya shule 45 zenye wanafuzi wenye mahitaji maalumu pamoja na wanafunzi wasioona na wenye uwezo wa usikivu hafifu, Serikali pia imenunua vifaa kwa ajili ya walimu kufundishia na vifaa hivyo ilivitumike katika kufundishia na kwaajili ya upimaji wa elimu ya mwanafunzi, aliendelea kusema waziri Mkuu

Hiki ni kielelezo cha dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Tano chini  ya ya Rais Wetu mpendwa Dkt, John Pombe Joseph  Magufuli ya kuhakikisha kila mtoto wa kitanzania mwenye umuri wa kwenda shule anapata huduma hiyo bila ya kujali hali hiyo

Vifaa vinavyo sambazwa vitasaidia kukuza kiwango cha taaluma kwenye shulezetu zenye wanafunzi wenye mahitaji maalumu na vilevile vitaongeza hamasa kwa watoto kupata elimu, alisema waziri Mkuu

Natowa wito na kuwasihi wazazi wote nchini tusikate tamaa na wala tusikatishwe tamaa ili tutimize ndoto za watoto wetuza kufika mahali wanapokusudia , jambo hili linawezekana kwa vijana hawa kupata elimu na wala tusiwafiche na Mh, Waziri hapa amesisitiza kwamba watoto hawa wasifichwe katika manyumba 

Nivizuri kutambua watoto wenye mahitaji maalumu ili liweze kuwa endelevu na  kwa Serikali hii inadhamira ya Dhati kutekeleza mahitaji ya wanafunzi hao

Serikali imedhamiria kuongeza maslahi kwa walimu na kudhamiria  kutwapa mafunzo ya mara kwa mara  kuendana na mitaala , nakuendelea kusema

Wizara ichukue hatua stahiki na kwawale wazazi wanao waficha watoto majumbani na wakibainika wazazi hao bazi hatua kali zichukuliwe juu ya mza au wazazi.  Mtoto akisha zaliwa siwako ni wataifa zima na nijukumu la Serikali kumuwekea mpango endelevu na kwahiyo agizo hili litekelezwe

Pia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametowa wito kusimami nidhamu kwenye eneo letu la elimu ili tujenge Taifa la wasomi na  kwa yeyote atakaye bainika kuharibu mwenendo wa mtoto wakike na aka mpa ujauzito mwanafunzi na ikibainika atakwenda jela miaka 30, awe mzazi kumuozesha mwanafunzi ati mnataka ,ng'ombe, mbuzi ,kondoo na ikibaanika jela miaka 30, au kumtorosha na kumpeleka chumbani kwako ni miaka 30, kuowa mwanafunzi miaka 30,Serikali imedhamiria kuwekeza katika kumlinda mtoto wa kike. sasa nitowe shukrani zangu kwa za dhati wote waliojiltolea katika kukamilisha hafla hii  na kuwashukuru Ilala na kuwaona vijana wa hamasa 

Pia Benk ya Duni, na wadau wote na viongozi wa elimu na kumshukuru Mkuu wa Shule hii  . Sasa nakwenda kuzindua rasmi




Baadhi ya vifaa vya kufundishia 


 Afisa wa Kituo cha Kitaifa cha Upimaji wa Kielimu, Mary Batamula, akitowa maelezo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe na baadhi ya  viongozi mbalimbali katika uzinduzi  wa ugawaji na usambazaji wa vifaa maalum kwa wanafunzi nchi nzima wenye mahitaji maalum uliofanyika Dar es Salaam jana,  kuanzia kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Uhuru Mchanganyika , Anna Mshana ,  Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako na kulia ni  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya ElimuSayansi na Teknolojia Dkt Leonard Akwilapo


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kulia) akimkabidhi baadhi ya vifaa  vya kufundishia Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko Mwalimu, Anna Mshana wakati wa uzinduzi huo Dar es Salaam jana


Baadhi ya wanafunzi wakisikiliza kwa umakini wakati Waziri Mkuu Kassim Majalia alipokuwa akihutubia




 Vijana wa hamasa wa Ilala wakiingia katika shule ya uhuru Mchanganyiko kabla ya Waziri Mkuu kuwasili Shuleni hapo

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages