LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 23, 2017

UVCCM YAMLILIA ALLY YANGA

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umepokea kwa fazaa, huzuni na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mshabiki mashuhuri wa Timu ya Dar es Salam Youngs African Ali Yanga aliyefariki katika ajali ya gari huko Mpwapwa mkoani Dodoma.

Aidha Umoja huo umeeleza kuwa kifo cha mwanachama huyo machachari kimeacha pengo na majonzi makubwa katika klab yake hususan katika uwanja wa soka la Tanzania. 

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka amemtumia salamu za mkono wa pole na rambirambi  Katibu Mkuu wa Yanga Charles Bojiface Mkwasa na kumuelezea masikitiko ya jumuiya hiyo kufuatia kifo hicho. 

Shaka katika taarifa yake ya hiyo alisema marehemu Ally Yanga licha ya kuwa mwanachama maarufu pia ni mwanajumuiya ya umoja wa vijana (UVCCM) ambapo katika maisha yake mara kadhaa amekuwa akishiriki na kushirikishwa  ipasavyo  hasa nyakati za kampeni na chaguzi kuu. 

Alisema akiwa mkoani  Dodoma alipata taarifa kupitia mitandao ya kijamii zikieleza kuwa Ally amepoteza maisha katika ajali ya gari na  kulazimika kuandika tanzia iliyokwenda mezani  kwa Katibu Mkuu wa Yanga katika Makao Makuu ya timu hiyo yaliopo kwenye  mkutano ya mitaa ya Jangwami na Twiga jijijini Dar es Salaam. 

"UVCCM imepokea kwa huzuni, majonzi na masikitiko makubwa kifo cha mwanachama huyo mashuhuri wa Yanga ambaye pia ni mdau na mwanachama wa UVCCM, Ally atakumbukwa kwa mapenzi yake makubwa kwa klab yake na kuwa mkereketwa kwa Chama Cha Mapinduzi "Alisema Shaka. 

Alisema katika maisha yake Ally alipenda ucheshi , masikhara, utani na uzungumzaji wa masuala ya soka huku akiipenda mno Yanga na inapofungwa hasa na watani wao Simba, aliweza hata kutokwa na machozi pamoja na kushindwa kula chakula

Kaimu huyo Katibu Mkuu alisema UVCCM ina wanachama wengi ambao ni mashabiki na wanachama katika timu mbalimbali nchini kama vile  Yanga, Kagera Sugar, Simba, Pan African,Small Simba, Cosmo Politan , Malindi, Pamba, Azam , Red Star, Mbeya City, JKT, Magereza na nyingine kadhaa .

"UVCCM katika soka kila mmoja yuko huru kuchagua na kushabikia timu anayoitaka na kuipenda, jumuiya yetu ina mkusanyiko wa wanachama na mashabiki wa Timu nyingi nchini wenye itikadi tofauti za kisiasa 'Akisisitiza Shaka 

Juzi mchana  Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo  na Ally akapoteza maisha.

Ally Yanga anakumbukwa kutokana na mikogo ilioambatana na mbwembwe zake kila Yanga ilipokuwa ikicheza. Alipenda sana mtindo wa kujipaka masizi meusi usoni mwake huku akiweka kitambi cha bandia.

Mungu amlaze mahali pema Ally Yanga.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages