LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 15, 2017

UVCCM WAMPA ZA USO LOWASSA.

Wamuambia ni Mkongwe wa kuzua mambo.

Mwandishi wetu, Dar Es Saalam. 
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM)  umemtaka  Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Rchmond Edward Lowassa kuacha uongo kwani hana historia ya kupigania maslahi ya umma.

Aidha, imesema madai ya lowassa kwamba   aliwahidi wananchi angeunda Tume ya kupitia mikataba ya madini kama angeshinda urais ni uongo na kutaka kujitafutia umaarufu wa kisiasa. 

Pia umoja huo umemtaka Lowassa kuonyesha ushahidi  video ya matamshi yake wakati  akiwa katika mkutano wa hadhara akihutubia mkoani Geita ikionyeaha kama kweli  alitoa matamshi hayo. 

Hayo yalielezwa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka alipozumgumza waandishi wa habari jana ofisini kwake Upanga jijini Dar Es Salam. 
alisema Lowassa hama nguvu za uzalendo wa kupigania au kuzungumzia mapambano dhidi ya ubadhirifu wa mali  za umma kwasababu hata kujiuzulu kwake kulitokana na shinikizo la bunge huku akihusishwa na sakata la ufisadi.

Shaka alibainisha kuwa hakuna  ushahidi wala kumbukumbu inayoonyesha kuwa Lowasa siku moja  aliwahi kutetea maslahi ya umma wakati akiwa serikalini kama Waziri au alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete. 

"UVCCM tumemestushwa na matamshi ya Lowasa yanayodai  wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu akiwa Mkoani Geita kuwa aliwahi kutamka kama angeshinda urais angeunda Tume ya kupitia mikataba ya madini , hakuna ushahidi huo na hawezi kuthibitisha ni uongo  mtupu "Alisema Shaka. 

Shaka alisema kama kweli angekuwa na ujasiri huo wakati alipokuwa waziri mkuu angeweza kutamka maneno hayo au kumshauri Rais iundwe Tume lakini alishindwa kwa sababu hana ujasiri na uzalendo kama anavyotaka kuwaaminisha wananchi baada ya kuona Rais John Magufuli akiungwa mkono kitaifa na kimataifa. 

Kaimu huyo  Katibu mkuu alikumbushia kuwa  alichosikika akisema Lowasa ni kwamba akiwa Rais atawakaribisha wawekezaji zaidi pamoja na marafiki zake wenye nguvu za fedha na mitaji mikubwa ili kuiendeleza migodi na uchimbaji wa madini ambayo itamtajirisha kila wananchi bila kuelezea mbinu za utekelezaji huo.

"Waziri pekee  jasiri, mzalendo na aliyekuwa mchapakazi kwa bidii katika serikali ni  Dk Magufuli kwani  hata Lowassa alipomnadi Dk Magufuli wakati akiwania ubunge mwaka 2005 alimtaja mbele ya wananchi kwamba ni jembe na turufu muhimu "Alisema Shaka. 

Aidha alieleza sifa peke ya Lowassa akiwa serikali ni tabia yake ya kumshauri jambo Rais na kama litafanyika, hugeuka na kuwaambia watu kwamba yeye ndiye akiyemshauri Rais na kama si yeye kisingefanyika. 

Shaka alisema upo ushahidi kwamba aliwahi kumshauri suala fulani  Rais  mstafu Mzee Ali Hassan Mwinyi kisha akawaambia wapambe wake kwamba yeye ndiye aliyeshauri kitendo  kilichomfanya Mwalium Julius K. Nyerere amwite kilichjambo lililomfanya mwalimu Julius Nyerere amwite Lowassa  nyumbani kwake msasani na kumkanya. 

"Lowasa aliitwa mbele ya  aliyekuwa Katibu Mkuu wa UVCCM Sukwa Said Sukwa nyumbani kwa mwalimu Msasani akasemwa  vikali sana na mwalimu kwa kitendo hicho pia akaonywa aache kutumia magazeti kusaka uongozi na umaarufu"Alieleza Shaka

Pia  Shaka alimtaka Lowassa kuacha tabia ya kutaka kuvika joho lisilo na hadhi yake na akumbuke  tuhuma ambazo amewahi kurushiwa na viongozi wa chadema wakipita huku wakimnadi nchi nzima haziwezi kufutika kwa mtindo anaotaka wa kujifagilia kwa uzushi. 

Hata hivyo kaimu katibu mkuu huyo alisema si kweli kama ujasiri, uzalendo na utashi wa kutaka kufanya mabadiliko ya kiuchumi, kupambana na ufisadi na kupitia mikataba michafu haiwezekani kufanyika bila  katiba mpya kama  anavyodai Lowasa. 

"Ujasiri, uzalendo na uthubutu wa kutenda mambo yoyote magumu hakuhitaji mabadiliko ya katiba , aidha kwa kuwepo wa katiba mbaya au nzuri kwasababu vitu hivyo havishabihiani , katiba iliopo ni nzuri na Dk Magufuli ataleta maajabu ya kihistoria chini ya katiba ya sasa "Alisisitiza Shaka 

Alimtaka Lowasa kufuta ndoto na matumaini  kwamba itatokea siku moja  akawa Rais wa nchi hii na kuacha kueneza uzushi kuwa alikatwa jina lake kwa kumhofia angepitia mikataba ya madini. 

"Jina la Lowassa liliondolewa kwasababu kadhaa ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka, viongozi wa CHADEMA kumnanga nchi nzima pamoja na ukiukaji wake wa  taratibu, miiko na maadili   huku akitumia nguvu za fedha kutaka ateuliwe  jambo ambalo CCM   imelikataa "Alisema Shaka .

Baadhi ya vyombo vya habari jana vilimnukuu Lowassa akimpongeza Rais Dk Magufuli kwa kuunda Tume ya kupitia mikataba ya madini huku akijigamba naye aliwaahidi wananchi wakati kampeni akiwa mkoani Geita kwamba akishinda urais angeunda Tume jambo ambalo pia lilifanya jina lake kukatwa ndani ya CCM.


Source Uhuru 15/06/2017


End

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages