Monday, June 26, 2017

RAIS MSTAAF ALI HASSAN MWINYI AFUTURU NA WATOTO YATIMA DAR

Rais Mstaafu awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (Kushoto) akichagua chakua anacotaka aliposhiriki na watoto yatima wa Kituo cha Kigogo kufuturu futari iliyoandaliwa na Kampuni ya  Bima ya AAR  jijini Dar es Salaam, jana.

Wageni waalikwa wakipakua futari.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Bima ya AAR wakiwapakulia wageni futari.
Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni ya Bima ya AAR, Agnes Batengas akiwangoza watoto kwenda kuchukua futari.

Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni ya Bima ya AAR, Agnes Batengas akitoa shukrani zake za pekee kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi baada ya kushiriki futari na watoto yatima wa kituo cha kigogo jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko na Mauzo Kampuni ya AAR Insurance Tabia Masoud akiwahudumia chakula watoto yatima kutoka Kituo cha Kigogo katika hafla fupi ya kufuturisha iliyofanyika jijini Dar es salaam.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi akitoa shukrani zake baada ya kushiriki futari na watoto yatima wa kituo cha kigogo iliyoandaliwa na kampuni ya Bima ya AAR.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya AAR, Violeth Mordichai akizungumza wakati wa hafla fupi ya kufuturisha watoto yatima wa Kituo cha Kigogo jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi akimkabidhiwa zawadi na Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni ya Bima ya AAR, Agnes Batengas wakati wa kufuturisha watoto yatima kutoka Kituo cha Kigogo jijini Dar es salaam jana.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Bima ya AAR wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima baada ya kuwakabidhi zawadi katika hafla ya kufuturisha watoto hao wa kituo cha Kigogo jijini Dar es salaam na kuwapa misaada ya chakula, nguo na viatu kwa ajili ya sikukuu ya Eid El Fitri.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.