LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 21, 2017

RAIS DK. MAGUFULI AMLILIA ALI YANGA

Rais Dk. John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia, wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), uongozi wa Klabu ya Yanga na wanamichezo wote kwa ujumla kufuatia kifo cha shabiki mkubwa wa timu ya Yanga Ali Mohamed maarufu kwa jina la Ali Yanga.

Ali Yanga amefariki dunia jana tarehe 20 Juni, 2017 kwa ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Chipogolo kilichopo katika Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, imesema, Rais Magufuli amesema Ali Yanga atakumbukwa kwa uzalendo na mchango wake wa kuhamasisha na kushabikia masuala mbalimbali ya kitaifa na hasa michezo, ikiwemo kuishabikia timu yake ya Yanga, timu ya soka ya Taifa, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na shughuli za kiserikali kama vile Mwenge wa Uhuru na ziara za viongozi.

“Nimeguswa sana na kifo cha Ali Yanga, nilikuwa nae wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ambapo alitoa mchango mkubwa katika uhamasishaji wa wananchi kukipigia kura chama changu cha CCM, na pia amekuwa akiongoza mashabiki wenzake kuishabikia timu ya Yanga na timu ya Taifa bila kuchoka. Kwa kweli alikuwa hodari sana katika ushabiki wake.

“Natoa pole nyingi sana kwa familia yake, viongozi wa timu ya Yanga, wanamichezo wote, wana CCM na wote walioguswa na kifo cha Ali Yanga na namuombea kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi, Amina” amesema Rais Magufuli.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages