HABARI MPYA

Your Ad Spot

Jun 19, 2017

POLEPOLE AFANYA MAZUNGUMZO UJUMBE KUTOKA KITUO CHA DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI CHA UHOLANZI, OFISI NDOGO YA MAKAO MAKUU YA CCM, DAR ES SALAAM, LEO

 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akimsalimia Meneja Mradi wa kushawishi Siasa Shirikishi katika kuimarisha vyama vya Siasa hapa nchini, hasa katika ushiriki wa Wanawake na Vijana katika masuala ya Siasa, unaoendeshwa na Kituo cha Demokrasia ya Vyama Vingi cha Uholanzi (NIMD) kwa kushirikiana na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD),  Arjan Van Der Waal, wakati alipokutana na ujumbe wa Meneja huyo na Mwakilishi wa NIMD Kanda ya Afrika Dk. Augustine Magolowondo (kulia), katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM,Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Watatu kulia ni Mwenyeji wa ugeni huo, Daniel Loyc kutoka TCD. 
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akimsalimia Mwakilishi wa Kituo cha Demokrasia ya Vyama Vingi cha Uholanzi (NIMD) Kanda ya Afrika Dk. Augustine Magolowondo kutoka Malawi, alipopokea na kufanya mazungumzo na ugeni huo kutoka NIMD, leo
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akiwakaribisha kuketi kwa ajili ya kuendelea na mazungumzo
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akizungumza na ujumbea kutoka Kituo cha Demokrasia ya Vyama Vingi cha Uholanzi (NIMD) katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. MAELEZO/PICHA NA BASHIR NKOROMO

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages