Tuesday, June 27, 2017

HUMPHREY POLEPOLE AKUTANA NA COUNSELLOR NA KATIBU WA BALOZI WA CHINA

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole jana, amekutana na Viongozi wa Ubalozi wa China na kuwa na mazungumzo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kujadili Mambo Mbali Mbali ya Kiutendaji kichama na Kiserikali.

Mazungumzo hayo yaliwahusisha Dong Zhenyu ambaye ni Katibu wa Balozi wa China Nchini Tanzania,
 Dai Xu Counsellor wa China Nchini Tanzania Pamoja  na George Daniel Afisa Idara ya Siasa na Uhusiano KimaTaifa na baadhi ya Watendaji Idara ya Itikadi na Uenezi.

Ugeni  huo  ulikuwa na lengo la kujifunza  uzoefu wa Chama Cha Mapinduzi kinavyoendesha mafunzo kwa Makada, Nafasi ya Chama Tawala Nchini Tanzania, Utendaji wa Chama, Uteuzi wa Makada katika kukitumikia Chama na Serikali.

Katika mazungumzo Polepole aliwafafanulia na kuwaelezea jinsi Chama kilivyokuwa kikitoa mafunzo mbali mbali tangu mwaka 1961 hadi  1991 wakati wa mfumo wa chama kimoja ambapo Chama cha TANU ndicho kilikuwa kinatawala baadaye CCM hadi sasa.

Polepole alitaja baadhi ya vyuo  vya mafunzo hayo kuwa vilikuwa  ni Kivukoni College Kigamboni- Dar Es Salaam, Lushoto -Tanga, Ilonga Kilosa, Hombolo- Dodoma, Msaginya- Rukwa, Murutunguru- Ukerewe na vyuo vyote hivyo vilikuwa ni vyuo vya mafunzo ya uongozi kwa makada na watendaji wa Serikali kuanzia Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kabla na baada ya Uteuzi. 

Counsellor wa Balozi wa China Nchini Tanzania Dai Xu alpongeza Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi kwa jinsi kilivyo na mfumo mzuri kwa kuwaandaa Makada na Viongozi katika kulitumikia Taifa la Tanzania.

Uongozi wa China Nchini  Tanzania kwa niaba ya Serikali ya China na Chama Tawala CPC umeahidi kushirikiana na CCM katika kuimarisha mafunzo kwa Vijana na Makada wa Chama Tawala ili kuendeleza Umoja na Mshikamano ulioasisiwa na Waasisi wa Mataifa yote mawili ya Tanzania na China.

PICHA: PETRO MAGOTI
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.