Saturday, May 13, 2017

UVCCM MWAMBUGU ALIKUA NI MWANASIASA MZALENDOMhe Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akisain Kitabu cha Maombolezo mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Said Mwambungu leo  wakati wa ibada ya kuaga mwili wa marehemu Said Thabit Mwambungu kabla kusafirishwa kuelekea kijijini kwao Malinyi Morogoro kwa mazishi .
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akisalimiana na Mhe Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya Mhe Rais Mstaafu kuwasili nyumbani kwa Marehemu Said Mwambungu leo  wakati wa ibada ya kuaga mwili wa marehemu Said Thabit Mwambungu kabla kusafirishwa kuelekea kijijini kwao Malinyi Morogoro kwa mazishi .
 Mhe Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akitoa Mkono wa pole kwa Familia ya Marehemu Said Mwambungu alipo fika  leo  kwa ajili ya ibada ya kuaga mwili wa marehemu Said Thabit Mwambungu kabla kusafirishwa kuelekea kijijini kwao Malinyi Morogoro kwa mazishi .
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akisain kitabu cha waombolezaji alipo wasili nyumbani kwa Marehemu Said Mwambungu leo  wakati wa ibada ya kuaga mwili wa marehemu Said Thabit Mwambungu kabla kusafirishwa kuelekea kijijini kwao Malinyi Morogoro kwa mazishi .
Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mery Majaliwa akisain kitabu cha waombolezaji alipo wasili nyumbani kwa Marehemu Said Mwambungu leo  wakati wa ibada ya kuaga mwili wa marehemu Said Thabit Mwambungu kabla kusafirishwa kuelekea kijijini kwao Malinyi Morogoro kwa mazishi .
  Baadhi ya waombolezaji wakiendelea kusoma dua mbali mbali za kumrehemu Marehemu Said Mwambungu.
Baadhi ya waombolezaji walio fika Msibani wakiendelea kusoma dua mbali mbali za kumrehemu nMarehemu Said Mwambungu.
Jenaza lenye Mwili wa Marehemu Said Mwambungu likiwa limefunikwa na bendela ya Chama cha Mapinduzi  pamoja na Baadhi ya waombolezaji wakiendelea kusoma dua mbali mbali za kumrehemuNyumbani kwake kabla ya kusafirishwa kuelekea kijijini kwao Malinyi Morogoro kwa mazishi .(PICHA NA FAHADI SIRAJI)


Na Mwandishi wetu. Dar Es Salam

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema umepata mshituko na fazaa  kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mwanasiasa na kiongozi jasiri aliyejituma kulitumikia Taifa lake kwa utii, nidhamu na bidii marehemu Said Thabit Mwambungu. 

Kaimu Katibu mkuu shaka Hamdu shaka ameyaeleza hayo nyumbani kwa Marehemu Said Mwambungu leo  wakati wa ibada ya kuaga mwili wa marehemu Said Thabit Mwambungu kabla kusafirishwa kuelekea kijijini kwao Malinyi Morogoro kwa mazishi .

Shaka alisema Mwambungu aliyezaliwa katika kijiji cha Malinyi Ulanga mkoani Disemaa 5 mwaka 1955 alianza kufanya kazi katika Umoja wa Vijana  wa CCM Machi Mosi mwaka 1978 na kuthibitishwa  kiajira Januari mosi mwaka 1979 akiwa katibu msaidizi Mkuu UVCCM Makao Makuu

Akiwa mtumishi hodari, makini na mchapakazi mahiri  aliteuliwa na Chama  cha Mapinduzi kuwa Katibu wa CCM wilaya ya Kibaha kabla hajapanda na kuwa katibu wa  ccm mkoa  wa Pwani. 

Shaka alisema kada huyo pia katika uhai wake aliteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa morogoro baadae akawa mkuu wa mkoa wa Ruvuma huku akiacha rekodi nzuri za kiutendaji katika nafasi zote alizowahi kushika kisiasa na kiserikali.

"Tumempoteza kiongozi shupavu, muaminifu na muadilifu, ameyatumia maisha yake kutumikia Taifa lake kwa utii nidhamu, ameanza safari ya utumishi akitokea UVCCM ambako alipikwa kimaadili na kizalendo "Alieleza Shaka 

Aidha Kaimu  Katibu Mkuu ameitaka familia marehemu, ndugu na jamaa kuwa wenye ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba na maombolezo kwani uamuzi na mapenzi ya mwenyezi mungu hayawezi kuepukwa na binadamu. 

Pia  katibu mkuu shaka ametuma  salamu  za rambirambi kwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli na kumtakia awe mwenye subira kwa kumpoteza mwanachama shupavu, mtendaji mahiri akiwa serikalini na kada wa CCM aliyepevuka kisiasa na kiitikadi .

"Tunatoa mkono wa  rambirambi kwa Mwenyekiti wa Chama chetu na tunampa  pole zetu kufuatia kifo cha mwenzetu ametutoka katika wakati tuliokuwa tulimhitaji na kumtegemea, mungu amlaze mahali pema na kumsamehe makosa yake " alisema shaka

Marehemu Mwambungu ambaye kitaaluma ni muandishi  wa habari gwiji, atakumbukwa jinsi alivyotoa mchango katika tasnia ya uandishi wakati akifanya kazi katika magazeti ya chama tawala Uhuru na Mzalendo kwa miaka kadhaa . katika kuaga mwili wa nyumbani kwake Tabata viongozi kadhaa wamehudhuria wakiwemo Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Jakaya Mrisho Kikwete, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mery Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga,  viongozi wa CCM na jumuiya zake, makada na wanachi mbali mbali.

Marehemu Said Thabit Mwambungu atazikwa kesho Malinji Morogoro baada ya sala ya alasiri. Mungu ailaze mahali pema peponi roho yake.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.