SIYANTEMI AKAGUA GHALA LA CHAKULA WILAYANI MONDULI

Katibu Tawala wa Wilaya ya Monduli Robert Siyantemi, Jumanne tarehe 23/05/2017 ametembelea ghala linalotumika kuhifadhi shehena ya mahindi ya serikali (kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Kanda ya Arusha - NFRA). 

Katika ziara hiyo Komredi Siyantemi amezungumza na Maofisa wa NFRA na baadhi ya watendaji wa serikali na kuagiza kuwa, zoezi hilo la uuzaji mahindi ya serikali kwa bei elekezi kwenye maeneo yenye ongezeko la bei linapaswa kusimamiwa kikamilifu kwa kufuata taratibu na miongozo. Wakati huo huo, Komredi Siyantemi amekagua utekelezaji wa zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa, linaloendelea wilayani Monduli.

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.