Tuesday, May 2, 2017

SHAKA AWATAKA VIJANA KUCHAGUA VIONGOZI SHUPAVU, WACHAPAKAZI

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Mpanda

Na Mwandishi Wetu, Katavi
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umewataka wanachama wa CCM kujitokeza  na kuamua kidemorasia kumchagua kiongozi yeyote mwenye sifa na anayefaa. 

Pia umoja huo umeeleza kuwa kila mwanachama ana haki ya kuchukua fomu na kuwania nafasi  ambayo anafikiri ana uwezo nayo katika kuwatumikia wananchma na chama kwa bidii na maarifa. . 

Shaka alitoa matamshi hayo jana wakati akizumgumza na baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa uliofanyika kwenye ofisi za ccm wilaya ya  Mpanda mkoani hapa .

Alisema kazi ya siasa ni ya kujitolea hivyo kila mwanachama anayechukua fomu kutaka kuwania nafasi yoyote atambue chama kinahitaji mtu mwenye juhudi , bidii na utii ili akijenge, kukitumikia na kukitetea kwa nguvu na hekima. 

"Huu ni wakati muafaka  wa kuwapa nafasi wanachama wetu katika ngazi zote kuamua nankuchagua kwa ridhaa yao, kuwapa viongozi  kwa hiari bila kushawishiwa kwa sababu za kujongwa , rushwa, ahadi au siasa za hadaa "Alisema Shaka. 

Aidha akizungunza ziara za viongozi wa chama na jumuiya mkoani na wilayani, alisema ziara hizo ni chama , viongozi wanapita ili kutazama uhai wa chama na maendeleo yake.

Shaka alisema anapokuja kiongozi wa chama katika mkoa husika jumuiya zote zinapaswa kushiriki katika hatua za maandalizi, kupanga na kushiriki  toka mwanzo hadi mwisho .

"Ziara zote ni za CCM,CCM ina junuiya zake, jumuiya ni watoto wa chama , chama chetu ni mfano wa mti wenye mizizi mirefu , matawi makubwa yanayotoa matunda , chama na jumuiya zake wote watoto wa mtu mmoja "Alieleza .

Kaimu huyo Katibu Mkuu alisems kazi za chama na jumuiya zake ni kuhakikisha uhai wa chama unaimarika, kuongeza idadi ya wanachama wapya  na kufanya kazi kwa bidii ili kihinde na kuongoza doka.

"Tuendelee na kazi ya kukipa uhai chama chetu, wsnanchi wanakiamini, wanakiamini na hawaoni chama mbadala nje ya ccm.,wajibu wetu ni kuwasemea  wananchi katika matatizo ysnayowakabili "Alisistiza Shaka
  kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka akifungua Shina la wakereketwa la mafundi baiskeli kata ya Majengo wilayan mpanda

  kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka akipiga ngoma ya NSIMBA na kikundi cha wa mama Nsimba
 Wanachama wa CCM Wilaya ya Mpanda wakishangilia katika Mkutano wa Ndani Wa kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka.
 Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa Haidar Sumri akizungumza katika mkutano wa ndani wa kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Katavi, Kajoro Vyohoroka.

  kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka akiagana na wananchi mara baada ya kumaliza Mkutano wa Ndani katika wilaya ya Mpanda Mkoani katavi.

  kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka akitoa jezi katika timu zilizo shinda kombe la MBOGO CUP kwa ufadhili wa Mbunge jimbo la Nsimbo.

  kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka akikagua Mradi wa  kilimo cha bamia wa Vijana wa kavicha uliopo kata ya kasokola wilayani mpanda picha na (FAHADI SIRAJI)
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.