LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 23, 2017

RAIS DK. MAGUFULI KESHO KUPOKEA TAARIFA YA MCHANGA WA MADINI ULIKO KATIKA MAKONTENA

Ikulu, Dar es Salaam
Rais John Magufuli kesho atapokea Taarifa ya Kamati Maalum aliyoiunda kuchunguza mchanga ulio katika makontena ya mchanga wa madini (Makinikia) yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini Tanzania.

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, imesema leo kwamba, tukio la kupokea taarifa hiyo litahudhuriwa na viongozi mbalimbali na kurushwa moja kwa moja kupitia vituo vya habari vya redio, televisheni na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz

"Wananchi mnakaribishwa kutazama na kusikiliza matangazo hayo yatakayorushwa hewani kuanzia saa 3.30 Asubuhi kutoka Ikulu Jijini Dar es Salaam", imesema taarifa hiyo.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages