Wednesday, May 31, 2017

RAIS DK MAGUFULI ATEUA MANAIBU GAVANA BENKI KUU YA TANZANIA

Ikulu, Dar es Salaam.
Rais Dk. John Magufuli leo Mei 31, 2017 amefanya uteuzi wa Naibu Magavana wawili wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Taarifa iliyotolewa na Ikulu imesema, Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Yamungu Kayandabila kuwa Naibu Gavana anayeshughulikia Uchumi na Fedha (Economic and Financial Policies – EFP) kuchukua nafasi iliyoachwa na Dk. Natu E. Mwamba ambaye amemaliza muda wake.

Taarifa imesema,  Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mtaalamu wa Uchumi na Fedha wa BOT Dk. Bernard Yohana Kibese kuwa Naibu Gavana anayeshughulikia Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha (Financial Stability and Deepening – FSD) kuchukua  nafasi iliyoachwa na Lila H. Mkila ambaye amemaliza muda wake.

Kwa ,ujibu wa taarifa hiyo ya Ikulu, uteuzi huu unaanza mara moja. 
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.