Wednesday, May 17, 2017

RAIS DK. MAGUFULI AMTEUA MKUU WA WILAYA YA MANYONI KUWA MKURUGENZI MTEDAJI WA KITUO CHA UWEKEZAJI TANZANIA (TIC)

Ikulu, Dar es Salaam
Rais Dk. John Magufuli amemteua Geoffrey Idelphonce Mwambe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijni Dar es Salaam, leo, imesema, kabla ya Uteuzi huo Geoffrey Idelphonce Mwambe alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida na kuongeza kuwa nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni itajazwa baadaye.

Taarifa imesema, wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Clifford Tandari kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, kuchukua nafasi ya Dk. John Ndunguru ambaye amestaafu.

Kabla ya uteuzi huo Clifford Tandari alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC). Uteuzi wa viongozi huo unaanza mara moja.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.