Wednesday, May 3, 2017

POLEPOLE: CCM IMEIAGIZA SERIKALI KUSAMBAZA TANI 1,500 ZA MAHINDI LONGIDO, NGORONGORO NA MONDULI KUKABILIANA NA UHABA WA CHAKULA

Na Irene Mdoe, Longido
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole amesema Chama Cha Mapinduzi kimeiagiza Serikali kusambaza tani 1,500 za chakula katika Wilaya za Longido, Ngorongoro na Monduli ili kukabilianana upunguzu wa chakula katika Wilaya hizo.

Amesema, CCM inachukua hatua hiyo kwa kuwa ni chama cha watu ambacho kimeundwa na watu ili kiwasemee, kuwatetea na kuwasimamia kutatua kero na changamoto, hivyo hakiwezi kujitenga na shida za watu.

Polepole alisema, hayo alipokutana na  viongozi wa Kata na Wanachama wa CCM katika Wilaya ya Longido mkoani Arusha ambapo viongozi na wana CCM hao walimuomba awasaidie ili kuweza kutatua tatizo la chakula linaloikabili Wilaya hiyo.

Walisema,  kutokana na uhaba wa chakula uliopo, debe la mahindi limepanda bei kutoka Sh. 5, 000/= hadi kufikia sh. 30,000/= huku gunia la mahindi hayo likipanda bei hadi kufikia sh. 150,000/= hadi sh. 200,000/= badala ya bei ya awali ya  ya sh. 45,000.

Polepole ambaye yupo katika ziara ya kuimarisha uhai wa Chama atakuwa mkoani Arusha hadi Mei 7, 2017, kabla ya kuendelea na ziara kama hiyo mkoani Manyara.
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.