Tuesday, May 2, 2017

MAKONDA NA MNYETI WASAMEHEWA NA BUNGE BAADA YA KUOMBA RADHI

Na Mwandishi Wetu
Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge la Tanzania, leo imewasilisha Bungeni taarifa za matukio mbalimbali ambazo imezifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuwaita na kuwahoji wahusika kwa kukiuka kanuni za Bunge nje na ndani ya bunge hilo.

Miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na ile ya kuingilia uhuru wa bunge kosa lililofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Bungeni, viongozi hao wote wawili wamesamehewa kutokana na kukiri makosa yao na kuliomba radhi Bunge la Tanzania.

Habarizimesema, Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imeazimia kuwasamehe Makonda na Mnyeti kutokana na kukiri na kujutia makosa yao na kuliomba radhi Bunge.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.