Monday, May 15, 2017

KIVUKO CHA MV NYERERE KUFUNGWA INJINI MPYA

Na Theresia Mwami
Serikali ina mpango wa kukifanyia matengenezo ikiwemo kukifunga injini mbili mpya, kivuko cha mv Nyerere kinachotoa ahuduma kati ya Bugorola na Ukara katika Kisiwa cha Ukerewe mkoa wa Mwanza.

Ahadi hiyo imetolewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu, baada ya kukagua utendaji kazi wa kivuko hicho na kushuhudia  kuwa kinazo changamoto ikiwemo kuhitaji matemngenezo.

“Tutanunua injini mbili mpya na kukifanyia matengezo ya kina kivuko hiki ili kuongeza zaidi ufanisi wake na hatimae kiweze kusafirisha abiria na mali zao kwa haraka zaidi na katika hali ya usalama mkubwa kwani injini zilizoko sasa zimechoka hivyo kushindwa kuendesha kivuko ipasavyo", alisema Dk. Mgwatu wakati akizungumza na wafanyakazi wa kivuko hicho.

Dk. Mgwatu aliwataka watumishi wa kivuko hicho kufanya kazi kwa bidii sambamba na kuziba mianya ya uvujaji wa mapato ya serikali, na kuzingatia weledi na uadilifu katika utendaji wa kazi.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

CCM Blog. Powered by Blogger.