Thursday, May 18, 2017

KINANA AONGOZA KIKAO CHA MAKATIBU WAKUU WA VYAMA RAFIKI NCHINI ANGOLA

Na Bashir Nkoromo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ameongoza majadiliano na viongozi wa vyama rafiki kikiwemo Chama Cha Kikomunisti cha China, vilivyoshiriki Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika.

Katika Mkutano Kinana amefuatana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga na Watendaji kutoka Jumuia za Chama Cha Mapinduzi.

Taarifa kutoka Angola, zimesema, katika Mazungumzo hay, vyama rafiki vimepongeza mabadiliko yalivyofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) hiv karibuni ambayo yamepewa jina la CCM MPYA, TANZANIA MPYA.

Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika ni pamoja na MPLA cha Angola, ANC cha Afrika Kusini, ZANU-PF cha Zimbabwe,  MPLA cha Angola, FRELIMO cha Msubiji, SWAPO cha Namibia na TANU ambacho sasa ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) cha Tanzania.
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.