Thursday, April 6, 2017

WASANII BONGO MOVIE WATINGA KWA MAKONDA AWAKOE NA JANGA LA WIZI WA KAZI ZAO


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na baadhi ya Watengenezaji na Wasanii wa Filamu nchini, baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake, leo. Panoja na Makonda ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro.
--------------------
NA BASHIR NKOROMO
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makaonda amewapa siku kumi wafanyabiashara za filamu kuhakikisha bidhaa hiyo wanaiuza wakiwa wameipata kutoka vyanzo halali ikiwemo ninavyohakiki maadili na ulipaji kodi.

Pamoja na hayo amesema pia ni marufuku mtu yeyote kuuza filamu zilizopakuliwa kwenye mitandao ya interneti, na kwamba kila bidhaa  ya filamu ni lazima iwe na nembo ya TRA, na zitakazokuwa hazina nembo hiyo zitachukuliwa kuwa muuzaji amezipata kwa njia isiyo halali hivyo atachukuliwa hatu.

"Na ili kuhakikisha hakuna anayeuza bidaa za movie za ku-download, mfanyabiashara atakayetaka kuingiza filamu za nje hapa nchini, tutamfuatilia ili kujua kweli ameziagiza kutoka nje na ameeziingia nchini kwa njia gani, hii itasaidia serikali kupata fedha kupitia kodi lakini pia itazuia kuingizwa nchini filamu zinazokiuka maalidi", alisema Makonda.

Akizungumza na Wasanii wa Bongo movie na watengeneza filamu hapa nchini, waliofika Ofisini kwake, leo jijini Dar es Salaam, Makonda alisema, kuwepo kwa wizi wa kazi za wasanii na kuwepo kwa filamu zinazokiuka maadili, ni miongozi mwa changamoto zinazotokana na utandawazi.

Mmoja wa wasanii waliofika kwa Makonda Jacob Steven (JB) alisema, kutokana na kuibiwa kazi zao, sasa wasanii wengi wa filam hawana fedha za kutosha kujikimu na hata kufanya kazi mpya za tasnia hiyo.

Alimuomba Makonda, kuwasaidia wasanii kwa kuwa wanaamini kutokana na uchapakazi wake ataweza kuwasaidia. "Tumeamua kuja kwako, baada ya kuona unavyopambana katika kulitetea taifa kwenye mambo yenye kulinda hadhi na maslahi ya taifa, hivyo tumeona hata kwa hili unaweza kutusaidia sana", alisema, JB.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na baadhi ya watengenezaji na Wasanii wa filamu hapa nchini alipofika ofisini kwake leo
Simon Mwapagata (kulia) akizungumza kuhusu kero ya kuibiwa kazi za wasanii na pia kupungua soko la filamu nchini kutokana na wauzaji ambao huzipakua kweneye mitandao bila gharama kubwa
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza huku Kamanda Sirro akimsikiliza kwa makini
Jacob Steven -JB akizungumza wasanii wa filamu waliovyoathiriwa na wauzaji wa kazi zao kiholela
Vincent Kigosi na Jenifa Kiaka wakiwa kwenye kikao hicho
Mwenyekiti wa Chama Cha Wasanii wa filamu nchhini, Jimmy Mafufu akizungumzia hali ya wasanii hao nchini
Paulo Makonda akizungumza
Picha ya pamoja
Wakibadilishana mawazo baada ya picha ya pamoja
JB akichukua namba ya simu ya Kamanda Sirro kushoto ni Innocent Kigosi-Ray
Jb akiagana na Makonda kabla ya wasanii hao kuondoka
Kigosi akihojiwa na mwandishi wa habari
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.