LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 27, 2017

WANAOPATA UJAUZITO KURUDI MASHULENI ASEMA WAZIRI UMMY

Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu akimuwakilisha Makamu wa Raisi Bi Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa  mkutano wa kwanza wa Masuala ya Usawa wakijinsia  ulioandiliwa na Chuo Cha Ualimu (DUCE) jijini Dar Es salaam
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesisitiza kuwa wanafunzi wa kike wanaopata mimba wakiwa mashuleni waendelee na masomo yao ili kufikia malengo walioyanayo nchini.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa maswala ya kijinsia ulioandiliwa na Chuo Cha Ualimu (DUCE) alipomuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri8 ya Muungano waq Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo jijini Dar es salaam.

“Tunapokataza watoto wa kike wasiendelee na masomo pindi wanapopata ujauzito wakiwa mashuleni  tunawaadhibu watoto wa masikini washindwe kutimiza malengo yao kwa wakati waliotarajia” alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa anaunga mkono uamuzi wa  Rais wa Tanzania Dkt. Jonh Pombe  Magufuli kwa  kutoa elimu bure nchini kwani kunaongeza idadi ya watoto wa kike  kuwepo mashuleni tofauti na kipindi cha nyuma.

Mbali na hayo Waziri Ummy ametoa wito kwa wazazi kuwahamasisha watoto wao wa kike kupenda masomo ya sayansi ili kukuza rasilimali watu katika kujenga uchumi unaotokana na viwanda nchini.

Kwa upande wa Mkuu wa Chuo cha DUCE Prof. William Anangisye amesema kuwa lengo la  mkutano huo ni kuleta chachu ya kuwatia moyo wanafunzi wa kike kupenda  masomo ya sayansi ili kupata  wanasayansi wanawake nchini.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages