RAIS DKT MAGUFULI KUWA MGENI RASMI MAADHIMSHO YA SIKU YA UHURU WA HABARI

Na Mwandishi Wetu
Rais Dk. John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Habari, yaliyopangwa kufanyikamwezi Mei mwaka huu.

Maadhimisho hayo ya mwaka huu, yatafanyikia jijini Mwanza kwa Siku mbili mfululizo kuanzia Mei 2 na 3 mwaka huu yakiwa na maudhui yanayosema 'fikra yakinifu kwa wakati muhimu'.

Akizungumzia madhimisho hayo, Mwenyekiti wa Misa Tanzania Salome Kitomary amesema lengo la siku hiyo ni kuwakutanisha wadau wa Habari kuweka msukomo wa mataifa kutunga sheria za vyombo vya habari ambazo zinahakikisha Uhuru wa habari katika nchi husika.

Amesema lengo lingine ni kufikia makubaliano ya kitaifa juu ya kuanzisha utaratibu wa usalama na ulinzi wa wanahabari na wafanyakazi wa vyombo vya habari kwenye mtandao na nje ya mtandao.

Kitomari amesema lengo lingine ni kutetea Sera na mfumo wa mageuzi ya kisheria kwa ajili ya vyombo vya Habari na maendeleo endelevu.

Kwa upande wake Makamu wa Rais kutoka umoja wa Clabu za waandishi Tanzania, UTPC, Janne Mihanji amewataka waandishi wawe ndio wapangaji wa ajenda za taifa badala ya kutumiwa na wanasiasa.

Aidha amewaasa waandishi wakiwa katika maeneo yao kazi, kuchukua tahadhari wakiangalia usalama wao zaidi kwani hakuna habari bora kuliko uhai wa mtu mwenyewe.

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.